CHASHA FARMING
JF-Expert Member
- Jun 4, 2011
- 7,872
- 9,263
Ushauri wa hovyo kuwahi kukutana naoMdogo wangu nikushauri kitu?
Maisha hayana formula, usikariri na wala usilazimishe vitu. Kwa sasa wewe ni mwanafunzi fanya uanafunzi. Utakapokuwa mjasiriamali utafanya ujasiliamali. Ukiwa mwanafunzi unatakiwa ufanye uanafunzi. Soma kwa bidii, nenda club, kesha library, hanagaika na masomo huo ndio uanafunzi. Usipofanya sasa amini nakwambia ipo siku maishani mwako utataka kufanya haya!
Wewe ni mwanafunzi wa udaktari unaogopa nini kuhusu ajira? Aliyekwambia madaktari hawana ajira nani au kwa kuwa unadhania kuajiriwa lazima uajiriwe serekalini?
Ikifika mahali pa ujasiliamali utafanya kaka. Usipindishe njia ya maisha. Enjoy uanafunzi wako, hakuna mashindano duniani kaka!
Sent using Jamii Forums mobile app