Nifanye nini niongeze kipato?

Nifanye nini niongeze kipato?

mdizi 2021

Member
Joined
May 4, 2021
Posts
55
Reaction score
52
Habari za asubuhi wana jukwaa, kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu. Mimi ni kijana nimeoa ninafanya kazi katika kiwanda kimoja hapa Dar, nina mkataba wa miezi 6 now imebaki 3 mkataba uishe. Tatizo ni kwamba mshahara ninaoupata ni mdogo kiasi kwamba hautoshi hata kwa mahitaji yetu muhimu.

Yaani napokea 180,000 kwa mwezi nikinunua chakula jumla na nikimuachia mke hela ya mboga jumla na madeni hela, mekata kodi nalipaga miez mitatu mi3 tu nashindwa kutoa michango ya kijamii hata hela ya kuweka akiba sina.

Sasa nimekuja humu mnisaidie mawazo nifanye jambo gani nijiongezee kipato au hata kunisaidia koneksheni ya kazi popote nitajilipua tu cha muhimu masilahi mazuri elimu yangu ni form 4 hali ni mbaya.

Natanguliza shukrani, Ahsanteni.
 
samahani mkuu nje ya mada hicho kiiwanda ninaweza kupata kazi kaka, maana mimi sina familia kwa kuanzia hyo tsh 180000 itatosha
Kwa sasa hivi uwezi pata kazi kutokana kuyumba kwa shughuli za uzalishaji
 
Ungekuwa na freezer shemeji angejifunza kufunga ice cream awe anauza mtaani , au mashuleni hiyo biashara Ina faida ingewapunguzia ukali wa maisha.
 
Back
Top Bottom