Nifanyeje ili kupunguza hasira?

Nifanyeje ili kupunguza hasira?

Una Miaka Mingapi?
Ukipatwa Na Hasira Kunywa Maji Au Kunywa Juice Ya Tikiti Maji.
 
wanajf naomba mesaada wenu. Ninatatizo la kuwa na hasira kupita kiasi hata kwa jambo dogo tu!

Cheki afya yako kama una shinikizo la damu.

Kuna mtu namfahamu alikuwa na hasira sana ila baada ya kugundulika ana shinikizo la damu na kutibiwa sasa hivi yuko kawaida!

Ila pia unapokumbana na tatizo lolote au mtu akikuudhi usikurupuke kuchukua hatua! Tuliza moyo kwanza.....baadaye utapata njia sahihi ya kulikabili.
 
ivi nyie mnaosema akae peke yake kumbukeni mleta uzi kasema ana hasira so kukaa peke yake I doubt anaweza kujitundika!
 
ka ma wewe ni muislam ukiwa na hasira kachukue udhu kisha pata rakaa mbili....yaani moyo wako utakuwa laini kabisa hasira zote zitapotea. ALLAH YAALAM.
 
Hata mimi nina tatizo kama hili yaani nina hasira za ghafla, lakini nimeplan nikijenga kajumba kangu nitaweka chumba maalumu kwaajili ya kukaa nikikasirika tena kutakuwa na kiti peke yake.
 
Dah unatatizo kama la kwangu mkuu. mimi pia huwa nakuwa na hasira za haraka sana na tiba yangu huwa ninakaa peke yangu sehemu tulivu kwa muda, maana zikipanda huwa sitaki kelele wala kusemeshwa na mtu.
 
utakuwa ni mjamzito ndo maana una hasira sana!
 
Hata mimi nina tatizo kama hili yaani nina hasira za ghafla, lakini nimeplan nikijenga kajumba kangu nitaweka chumba maalumu kwaajili ya kukaa nikikasirika tena kutakuwa na kiti peke yake.

Hahahahaaaaaaaaaaa
 
Unamuhitaji Mungu mwenyewe akubadilishe kupitia Yesu Kristo. Tafuta msaada wa kiroho hutajuta.
 
Unamuhitaji Mungu mwenyewe akubadilishe kupitia Yesu Kristo. Tafuta msaada wa kiroho hutajuta.

were unaweza kuwa ni Scorpio hiyo ni hulka haina dawa ni kuenda nayo na mazingira tu! Mimi Niko hivyo na sasa Nina umri wa miaka 64 naenda na hali hivyo hivyo kikubwa jifunze kudharau mambo mengi.
 
wanajf naomba mesaada wenu. Ninatatizo la kuwa na hasira kupita kiasi hata kwa jambo dogo tu!

Kila unapo shikwa na hasira jiulize UNAPATA FAIDA GANI. Ujue kwamba hasira ni hasara na huwezi kulitatua tatizo ukiwa na hasira, na pia watu watakukimbia..
 
Back
Top Bottom