Nifanyeje ili nilale usingizi wa bila mawenge!?

tindikalikali

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2011
Posts
4,854
Reaction score
1,129
Wadau kwa muda sasa nashindwa kulala vizuri, yani nalala kwa mawenge na hofu kubwa ni wezi/kuibiwa!!

Nipo katika uchumi wa kawaida tu ila usiku lazima nitashtuka na muda mwingine naamka kuchungulia dirishani na hata kwenda sebuleni!! Akili ikikaa sawa ndo nagundua kwamba ni wenge tu!

Nimejaribu kujilazimisha kurelax na kuzoea vitu nilivyonavyo lakini wapi, japo nyumba ina grills mlangoni, dirishan na madirisha ni ya vioo lakini bado naishi kwa hofu!

Naomba msaada wenu kipi nifanye ili nami nipate usingiz mzuri na siyo huu wa mang'amng'amu!!
 
Sijajua kinachokuzingua ni mali au ni woga tu wa kawaida.

Kama ni mali unaziwazia sana, umepotoka maana hujui chenye thamani maishani sio hizo mali. Ni hiyo akili, afya na utimamu wa kuendelea kusakanya.

Kama ni hofu za kawaida na kuota maruweruwe, kagua chumba chako km hewa ipo ya kutosha. Pia ulalapo, kichwa kielekee Kaskazini.

Hewa hupeleka oksijeni ya kutosha ubongoni hivyo ubongo kuliwazika. Kichwa kuelekea Kaskazini hufanya mwili uwe na mwafaka na nguvu sumaku za dunia hivyo kuliwazika.
 

Aisee hiyo ya kulala kuelekea kaskazin sikuwahi ijua kabla, kitanda kimeangalia magh/mash..na kulingana na chumba kilivyo siwezi kukielekeza kaskazini!!

Mkuu najua mali zinatafutwa, najaribu sana kuona nione ni kawaida..lakini ikifika usiku sijui akili huwa inapatwa na nini!?
 
tindikalikali, kugeuza kitanda haishindikani. Ikiwa chumba hakitatosha, basi fanya uhame chumba/nyumba.

Unatumia karibu theluthi ya maisha yako kitandani/chumbani. Hakikisha pana 'energy' na kitanda kina mwafaka.

Tofauti na hapo, hizo mali pia zitapotea maana itafika mahali unachangayikiwa kabisa unakosa uwezo kuzifatilia.

Bongo wengi tunaishi kwa kubahatisha. Jaribu hii kanuni ya kufata mwafaka wa dunia kisha utanambia.
 
Last edited by a moderator:
NAMNA YA KUPATA USINGIZI MZURI

1. Lala kwenye chumba chenye ubaridi kidogo - Usiku dunia huwa inapoa wakati mchana inapata joto zaidi. Ubaridi unasaidia kuleta usingizi mzuri.

2. Lala kwenye chumba kilicho na giza la kutosha/usiwashe taa chumbani - Usiku dunia (asili) huwa ina mwanga mdogo/giza.

3. Fanya mazoezi ya kukufanya uchoke kidogo. Kukimbia (Jogging) kwa nusu saa ni moja ya zoezi linalosifika kusaidia kuleta usingizi mzito.

4. Zima simu au redio wakati ukilala. Pata utulivu wa kutosha bila ya kusumbuliwa na simu au kusikiliza redio/tv.
 

Asante mkuu..itabidi nianze mazoezi maana nimekuwa mvivu sana siku hizi!!
 

asante mkuu umenipa mwanga!!
 
Last edited by a moderator:
Kinachokupa mawenge labda hizo mali umezipata kwa njia zisizo halali. Kwa hiyo roho ya uzurumati inakuandama.
 
Mkuu Tindikali weka Kipande cha Tangawizi chini ya mto hutoota ndoto mbaya. Ukitaka dawa ya kujikinga na Wezi na Wachawi Wasiweze kuingia nyumbani kwako Dawa mimi ninayo ukitaka nitafute mimi kwa kubonyeza hapa.Mawasiliano

MAGIC USE GINGER ROOT



JAMAICA GINGER, also calledJAKE ROOT, or AFRICAN GINGER, gives a fiery form ofProtection and heats up Love and Money Spells. A whole dried

root will protect from evil spirits, bad dreams, and hag-riding if kept under the pillow.
Powdered

GINGER
sprinkled in the yard stops trouble. Add driedGINGER to love oils and powders to increase the

heat of
Passion. A famous "Trio-Hand" forGambling consists of a whole GINGER ROOT, a whole John the Conqueror Root, and a whole Nutmeg. Each curio is

separately prayed over with the 23rd Psalm as it is anointed with
Fast Luck Incense Powders. The

assembled "trio" is then prayed over collectively, "In the name of God the Father, God the Son, and God

the Holy Ghost," before being placed in a red bag. We make no claims for
GINGER ROOT, and sell as a Curio only.
 
asante mkuu umenipa mwanga!!

Usijali. Ila usisahau mrejesho. Ndani ya siku 7 tu za kwanza usingizi utaimprove sana. Baada ya siku 90 hivi, nyanja nyingi za maisha yako zilizokua zikisumbua bila wewe kujua utaona zimeboreka sana.
 
Fanya kazi ngumu mchana kutwa uone utavolala kama mfu.
 

Kwa kumuongezea tindikalikali, hapo namba 3 yapaswa mazoezi uyamalize walau masaa 4 kabla ya kulala. Maana yake, ukimaliza mazoezi, yapite walau masaa 2 ndipo ule. Na ukimaliza kula, yapite masaa walau ma2 ndipo ulale.

Na katika kula usiku, epuka sana kushiba 'full' kama mchana. Ikiwezekana, na kama afya si mgogoro, yafaa usile kabisa usiku (hapa najua ni mgogoro kwa wengi - wazia bia bila supu mingi au nyamchom kwa sisi wa Chuga)!!
 
Last edited by a moderator:

usikose biringanya ktk mlo wako wa usiku, ni dawa ya usingizi ya asili na haina madhara
 
Bila Radio siwezi kulala...Lazima nifungulie Radio1 chombeza time na revocatus kimwaga.
 
Usishibe sana wakati wa usiku. Kula chakula angalau masaa 2 kabla ya kulala. Baada ya saa moja baada ya kula kunywa maji hata glasi tatu..Utalala tu. Mi hii imenisaidia sana.
 
ni woga wako... halafu yawezekana hata unanatatizo ya kuafya yansyokufanya uwaze sana na ubongo umechoka sasa....

wewe relax..acha uoga, jikubali jinsi ulivyo, hakuna uchawi hapo, we kabla ya kulala omba Mungu akulinde, usije ukasubutu kufanya aina yoyote ya tambiko kwa ajili ya ulinzi, Mungu pekee anatosha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…