Nifanyeje ili nipate ujasiri wa kupima HIV?

amua kutoka moyo na uweke akili yako sawa kupokea maamuzi hayo ya moyoni nautaweza
 

Mmh! Na we jamaa ni kiwembe kweli, lazima ubadilike, Kila mtu tu unatembea nae, utafupisha maisha yako ndugu
 
Hatua ya kwanza ilikuwa hiyo ya kuwaza kupima, hongera kwa kuruka kihunzi namba moja.

Hatua ya pili ni kuchukua hatua ya kwenda kupima. Ukifika pale utapewa ushauri nasaha na kuambiwa faida lukuki za kupima. Ili uchukue hatua, unapashwa kufahamu kuwa hiv sio death sentence anymore. Kuna watu lukuki wamekaa na ugonjwa up to 20+ years kabla hawajaanza kuumwa na kutumia dawa. Ukijua hali yako kwamza kihoro kitakuisha. Hakuna kitu kibaya kama haya maisha unayoishi ya kukohoa tu unawaza kama ndio ngoma.

Nenda kwa ushauri, kupima sio lazima. Utakapojisikia utaendelea na hatua ya kupima. Kuna uhuru wa ajabu baada ya kupima.
 
Mpe demu wko mimba, akijifungua, majibu ya clinic ndo majibu yko.
 

"You can fool some people sometimes.
But you can't fool all the people all the
time."--Bob Marley
 

Sidhani kama kuna ukweli wowote hapa..........yaani wote unaotembea nao wamepima hawana sasa iweje wewe uogope kwenda kupima???!!!! Mchukue mmoja kati ya hao uende nae atakupa nguvu na matumaini wakati unasubiria kujua status yako. Kama vipi niambie nikusindikize,mie siogopi hata!!
 
Aiseeeee babaangu we umeshaambukizwa ukimwi so usijisumbue
 

Pole sana. Ungewaachia namba ya simu wakutumie kwenye meseji
 
Ole wao wafanyiao umbea miili yao,maana majibu watakayopata yatawaharakisha kuiaga dunia hii na kukosa raha walizojaaliwa.Nzagamba 12:6

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Nunua home test kit ( I think inaitwa bio line test), fundishwa namna ya kujipima na kusoma majibu kwa usahihi. Then on sunday after church kula viroba vya kutosha upate confidence but do not over drink. Ole wako ukosea kujipima na majibu yaonyeshe una ngoma wakati huna, utajuta.!
 
Acha woga mtoto wa kiume! Nakushangaa unaogopa kupima HIV, je unaogopa nini kuchukua majibu? Inafaa nini kuwa na mwili bila kuwa na uhakika wake?
Nenda kesho kapime HIV, pima pia na homa ya ini (Hepatitis B). Usisikilize kauli za kizamani kama kupima hakuna faida, ni kujipunguzia muda wa kuishi n.k.
 
Tumia ujasiri ule ule ulioupata wakati unafanya ngono bila kinga!
 
Mkuu Episodes!

Kama roho inasita usijaribu kupima!
kuna watu humu jamvin wanataka wakudanganye
 
Mkuu siku unaenda nistue tuende wote, manake hata mimi kila kukicha napoteza ujasiri wangu wa awali.
Siku nikipata huu ujasiri na nikakuta sina ngoma, lazima nitoe mshahara wa mwezi mzima kama sadaka...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…