mtz daima
JF-Expert Member
- Apr 15, 2015
- 1,561
- 579
hakuna kitu kinanipa shida kama kwenda kupima afya yangu na kuijua afya yangu,nimejitahidi sana kujipa moyo lakini nashindwa kabisa kupata ujasiri wa kupima,nakumbuka mara ya mwisho pale mbeya nilikwenda kupima lakini wakati wa majibu nilipotea na sikupenda kurudi kwenye kituo tena,jamani kuna njia yoyote ya kuniwezesha nipime afya yangu?japo ni bure kupima lakini nimekosa ujasiri,hii ni mara ya pili naleta hii mada humu ndani kuhusu HIV,naomba washauri au wale ambao mliweza kupima mnisaidie ushauri kwani naweza kushawishiwa na ushauri wenu hapa jf kwa kuwa mimi ni msomaji mzuri wa mada za jf
naomba mliopima na kukutwa na virus mniambie yaliyowakuta siku ile baada ya kupewa result
na wale mliopima mkakutwa hamja athirika naomba mseme mlijisikiaje??
Mkuu huhitaji kuwa kuogopa mimi nimetoka leo hapa nasubiri wanitumie majibu kwa email yangu take it easy ni kama unavyopima maleria tu