Kwanza pole sana Mkuu,
Nikiunganisha na uzi wako wa kuwa na hasira, na kama unayoyasema ni ya kweli, basi inaonekana una tatizo kubwa ambalo linasababisha hayo yote. Of course, kuna wakati mtu unakuwa na hasira au unajisikia kutaka kuwa peke yako au kutoongeleshwa na mtu yoyote lakini ikiwa kila mara au kwa muda mrefu, basi hapo kutakuwa na tatizo.
Unafanya kazi? If so, kazi yenyewe ina ma-stress? Unatumia madawa yoyote? Unavuta sigara? Unakunywa pombe? Una uhusiano mzuri na ndugu zako? Uhusiano wako wa mwisho kimapenzi uliishaje? Maisha yako ya utotoni yalikuwaje? Umelelewa na wazazi wako wote (baba na mama)? Unashiriki kwenye michezo ya aina yoyote au kufanya mazoezi? Hayo ni baadhi tuu ya maswali machache ya kujiuliza.
Whaever the cause ni bora ukamwone daktari. Inawezekana una metabolic disorder, hypoglycaemia au ni tatizo la kisaikologia tuu, lakini ni bora hilo likadhibitishwa kitaalamu.
Vitu kama hasira ni mbaya sana. Kuna watu wameshauri tafuta mwanamke lakini kwa vile unapata hasira ni bora kwanza utatue hilo tatizo. Ikiwezekana kaa mbali kabisa na wanawake. Huwezi jua. Hasira zinaweza kukufanya bila kujua kumwa-abuse (sexual abuse) huyo mwanamke, kumpiga, kudhuru mwili wake au hata kusababisha kifo na kufanya hali iwe mbaya zaidi.
Kamwona daktari atakupa direction kwa wataalamu wanaweza kukusaidia.