Nifanyeje maji yatoke sikioni?

Nifanyeje maji yatoke sikioni?

hayolae

Senior Member
Joined
Sep 28, 2015
Posts
180
Reaction score
865
Jana mida ya sa nane mchana maji yaliniingia sikioni.
Mpaka sasa sikio moja la kulia limeziba.
Naombeni msaada nifanye nini ili maji yatoke nirudi kwenye hali angu ya kawaida?
 
Yatakauka yenyewe na kugeuka uchafu.

Halafu sijui huwa mnajua matumizi ya "news alert"?
 
Jana mida ya sa nane mchana maji yaliniingia sikioni.
Mpaka sasa sikio moja la kulia limeziba.
Naombeni msaada nifanye nini ili maji yatoke nirudi kwenye hali angu ya kawaida?
Unaishi wapi? Kama uko Dar nenda Ekenywa Dispensari ya Marehemu Dr Ole utakutana na ENT Specilist watakupa msaada.

Dispensari hiyo iko Magomeni Mwembe chai karibu na Shehe Tabata ni ya Ghorofa kama tano au sita hivi.
 
Ingiza maji ya uvuguvugu kwenye sikio lililoziba,
Geuza shingo upande wa pili ili sikio lililo na maji lielekee juu kwa dakika kama mbili hivi,
Baadae gandamiza kiganja cha mkono kwenyesikio lenyemaji ,inamisha chini sikio lenye maji huku ukiwa umeliziba kwa kiganja ili maji yasitoke.
Ondoa kwa kasi kubwa mkono wako ili maji jatoke kwa msukumo.

Rudia mara mbili au tatu zoezi hilo hadi mtaro wa sikio uzibuke.
 
yaongeze then zungusha kichwa kwa nguvu . Yote yatatoka kabisa
 
Pole ruka ruka haraf inamisha pemben ckio lenye maji yatatoka yote.
 
Unaishi wapi? Kama uko Dar nenda Ekenywa Dispensari ya Marehemu Dr Ole utakutana na ENT Specilist watakupa msaada.

Dispensari hiyo iko Magomeni Mwembe chai karibu na Shehe Tabata ni ya Ghorofa kama tano au sita hivi.
Lipia tangazo mkuu
 
Lipia tangazo mkuu
Ametoa maelekezo ya wapi anaweza kupata msaada, na sio Tangazo, na msaada aliomwelekeza ni wa kitaalamu, naheshimu mawazo ya wengine kwa kua yametokana na uzoefu wao, ila ni kubahatisha na unaweza usijue kuna uharibifu gani unaweza tokea kutokana na usalama mdogo wa njia husika ktk kutatua tatizo lako
 
Back
Top Bottom