Nifanyeje nipende mpira wa miguu


Arsenal imeingiaje hapa?

Nyie ndio wale mashabiki wa lile litimu linalopaki basi linaharibu utamu wa mpira.
 
Wewe jamaa umeandika vile nilivyo
 
Wakuu habarini, huwa naona watu wakishangilia kwa furaha wengine hata kula Hawali kisa mpira nifanyeje niupende mpira
Wala hupo peke yako ndugu, tupo wengi tu. Nimefanya kila mbinu but nimeshindwa. In short starehe yangu ni vitamin music na vitamin movies.
 
Ata mm..yan me na mpira ni vitu viwili tofauti..ata nikickia watu wanashangilia moyoni nashangaa sana..wangu music tu.
 
Mimi pia nitatizo la kutokupenda filamu za kibongo,nikikuta wanatazama bila hata kuuliza niya lini,huwa naondoka.
 
Wakuu habarini, huwa naona watu wakishangilia kwa furaha wengine hata kula Hawali kisa mpira nifanyeje niupende mpira
Fanya amka asubuhi tafuta mpira wa doso anza na danadana kisha kupigiana ,gombania goli,cheza funga duka ,one touch lazima utapata raha hapo sasa ukishakukolea hamia kwenye jabulani mtafute iconic star wako umuangalie anafanyaga nn na ww ufanye hivyo hapo utaupenda maana huwez kupenda kitu usichokiweza kukifanya
 
mpira nilikuwa nikicheza Sana nikiwa kijana mdogo , tulikuwa tukicheza mipara ya kufuma na kamba na kucheza danadana Lakin nashindwa kuelewa sipendelei kuutazama
 
Ingia youtube andika Lionel Messi skills, naamin utakachokutana nacho huku utakuja kuniambia then tafuta timu anayochezea, hakika utafurahi, BARCELONA OYEE
 
Daaah binafsi mpira umenishinda mazee
 
Haupo peke yangu ndugu, yaani mimi nimetumia kila aina ya style kusudi niupende mpira lakini ndio kwanza siuelewi kabisa nakujiona kama napoteza muda wangu,

Marafiki zangu wengi wanapenda mpira wakanishauri niwe nahuzuria kwenye mechi mbali mbali na pia kuangalia mipira kwenye tv nk itasaidia kunifanya niwe napenda mpira, nilifanya hivyo kila inapotokea mechi uwanjani au hata kwenye tv basi jamaa yangu akawa anaambatana nami popote kwenye mpira , yaani zaidi nikawa naona kero kwani sikuona furaha yoyote kutazama mpira sasa baadae nikaona mpira sio hobby yangu nikaamua kuacha kujihusisha na kitu nisicho kipenda , basi hadi leo nipo tu na ma hobby yangu mengine na maisha yanafuraha sana tu ,

Hivyo kama umejitahidi vya kutosha kupenda mpira na imeshindikana basi achana nao tu , utapenda vingine na maisha yataendelea poa
 
Wakuu habarini, huwa naona watu wakishangilia kwa furaha wengine hata kula Hawali kisa mpira nifanyeje niupende mpira
Hujaumbwa ufanye kila kitu chini ya jua,wala ujue kila kitu chini ya mbingu.km huna hobby basi acha tu maana angalia kusudi.ukilazimisha kuingia huoko utakufa utawaacha wanashangilia wale ulio wakuta
 
hata mm mpira umenipitia mbal asee,,nashangaaga sana vile watu wanakuaga excited asee
 
Ukitaka uupende mpira anza kubet, nakuhakikishia mpira utakuwa unafuatilia mpaka ndondo za ulaya
 
Kuangalia mpira. Kucheza fifa. Nilishindwa kabisa, ila nina timu zangu huwa zikifungwa roho inauma zikifunga nafurahi sana. Mpira wangu ni matokeo ya mechi tu
 
Achana na hiyo kitu ni ulevi wa hatari
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…