Hakuna mtu anayejilengesha kwako, ni wewe ndiye mwenye njaa ya ngono na unatumia shida zao kama fursa.
Hao unaodai wanajilengesha hujui mioyo yao ina siri gani. Wengine wana changamoto kubwa za kisaikolojia, na wengine wana magonjwa ambayo huwezi kuyajua kwa kuwaangalia usoni tu. Mtumishi wa afya mzima unajisogeza kwenye mtego wa kupata sexually transmitted infections kirahisi namna hiyo kwasababu tu ya tamaa ya muda mfupi, huu ni utoto, ujinga na kukosa akili ya maisha.
Kumbuka tu kuna law of Karma. Fikiria siku mkeo, dada yako, au binti yako wa kumzaa akifanyiwa uhuni huu huu na mtumishi mwingine wa umma kwasababu tu ana shida na anahitaji msaada utajisikiaje wewe? Huoni kwamba unajitengenezea laana wewe mwenyewe na kizazi chako kwa tabia hii?