TheChoji
JF-Expert Member
- Apr 14, 2009
- 5,771
- 17,849
Tangu nimehamia hapa mtaani ni takribani mwaka sasa umekatika. Mtaa ninaoishi ni nje kidogo ya mji ambapo watu wamejenga nyumba zao wamezungusha fensi na mageti. Pia wengi (pamoja na mimi) ni wafanyakazi ambapo mara nyingi ni watu wa kutoka asubuhi na kurudi jioni wakiwa ndani ya magari yao.
Sasa leo nimekaa nikatafakari, nikagundua kuwa zaidi ya majirani niliopakana nao upande wa kushoto na kulia, hakuna jirani mwingine ambaye walau hata namjua kwa jina. Hakuna mawasiliano ya aina yoyote kati yangu na majirani zangu, hakuna tukio lolote linalotukutanisha na hata ikitokea mtu akapata tatizo, sidhani kama kuna mtu atajitokeza kusaidia.
Mimi naona kama hii hali sio nzuri ila nashindwa kujua nifanyeje ili kujenga ujirani mwema, hasa kwa hawa majirani wa mbali kidogo nyumba ya tatu ya nne huko?