Nifanyeje nizoeane na majirani?

Nifanyeje nizoeane na majirani?

Utashangaa jirani na mbali zaidi wote wanakufahamu wanakuangalia tu. Nikupe incident tatu zimetokea nikajua kumbe watu wanakuchora tu
1.niliharibikiwa na gari mbali kidogo na home nikachukua bajaj kurudi home kutafuta alternative, yule wa bajaj akaanza kukata mitaa nikamuuliza wewe unajua unapoenda? akasema blaza si unakaa pale pako hivi na hivi...nikaishiwa pozi
2.Nimeenda dukani hardware kununua vitu sasa nataka mtu apeleke nyumbani mimi naenda kazini, kaitwa bodaboda akapewa nampa maelekezo ananiambia aah blaza si kwenye kona pale hivi na hivi!
3.wengine nimekuta masela wanaziba mashimo barabarani wakaniwahi blaza wa pale hivi na hivi tutoe leo pozi likaisha
Yaani watu wote wanakufahamu unapokaa,unaendesha gari gani etc ila unapita huongei na mtu wanakuangalia tu. siku moja moja shusha kioo wasalimie watu mtaani.
Itakuwa unamiliki kiberiti mkuu...maana watu wenye kiberiti wanajulikana sana[emoji848]
 
Sasa yeye si kajimix, ila hili tatizo hata mie ninalo siwezagi kuzoeana na watu kizembe wa mtaani! Sipendagi tu yale mazoea ya kujuana juana sana
Kama mimi inaniwia vigumu mnoo...sema ndugu zangu niko nao mtaa mmoja

Kwa majirani nimebagua kuna mmoja huyo mmama anajifanyaga ananijuuua kila mtu anampa habari zangu, nikamfungia vioo mwaka wa nne huu...wengine tunapeana hi tu
 
Tofauti na huko mbele, huku kwetu ukimkaribisha jirani kwako pamoja na kufaidika kwa fadhira zako, anatumia ku-scan nyumba yako nje ndani baada ya siku kadhaa unapata ugeni wa majambazi usiku mwigi.😀
Kabisa[emoji848]
 
Kama mimi inaniwia vigumu mnoo...sema ndugu zangu niko nao mtaa mmoja

Kwa majirani nimebagua kuna mmoja huyo mmama anajifanyaga ananijuuua kila mtu anampa habari zangu, nikamfungia vioo mwaka wa nne huu...wengine tunapeana hi tu
Una raha kukaa mtaa mmoja na ndugu zako
 
Njia rahisi ni kutembelea vijiwe ambavyo unadhani utakutana nao! Kama kuna Car wash mtaani jimix hapo weekend nunulia vijana soda mpige soga! Kama kuna ka duka mahali unaweza pata hata mtindi ukawa unapiga piga story na watu maeneo hayo! Kama ni mtu wa dini jiunge na jumuiya uwe unakutana na wenzio kila weekend.
Ila pia kuzoeana kwa mtindo huo ni hatari sana...yaan we unaona unaongea nao fresh nini sijui kumbe mtu anakuchora anataka akujue weakness na strengths zako akugeuze asusa...humo humo kwenye majirani kuna majambazi ujue[emoji848]
 
Ila pia kuzoeana kwa mtindo huo ni hatari sana...yaan we unaona unaongea nao fresh nini sijui kumbe mtu anakuchora anataka akujue weakness na strengths zako akugeuze asusa...humo humo kwenye majirani kuna majambazi ujue[emoji848]
Heheheh ndio nasema usiruhusu mazoea yaliopitiliza wala usifungue mafaili yako! Wawe wanakuona tu, ishi nao vizuri tu!
 
Tangu nimehamia hapa mtaani ni takribani mwaka sasa umekatika. Mtaa ninaoishi ni nje kidogo ya mji ambapo watu wamejenga nyumba zao wamezungusha fensi na mageti. Pia wengi (pamoja na mimi) ni wafanyakazi ambapo mara nyingi ni watu wa kutoka asubuhi na kirudi jioni wakiwa ndani ya magari yao.

Sasa leo nimekaa nikatafakari, nikagundua kuwa zaidi ya majirani niliopakana nao upande wa kushoto na kulia, hakuna jirani mwingine ambaye walau hata namjua kwa jina. Hakuna mawasiliano ya aina yoyote kati yangu na majirani zangu, hakuna tukio lolote linalotukutanisha, na hata ikitokea mtu akapata tatizo, sidhani kama kuna mtu atajitokeza kusaidia.

Mimi naona kama hii hali sio nzuri ila nashindwa kujua nifanyeje ili kujenga ujirani mwema, hasa kwa hawa majirani wa mbali kidogo nyumba ya tatu ya nne huko?
mi majiran niliwajua baada ya kwenda jumuiya. then kanisan coz enz hzo waumin tuko wachache basi ilibid tujuane.
 
Watu wanaweza wakakuogopa kwa class uliojiweka ila ukiwa bro mchangamfu hata vijana watakupenda tu hapo mtaani! Weekend egesha hata car wash, tia nao strory mfano kuna mwana ni engineer life safi ila anachezaga draft na wana kitaani tu on weekends. Anazungusha kahawa bill kwake maisha yanaenda na anajulikana freshi!

Watu wakuzoee ila sio ile sana mpaka mtu anajua unafanya kazi wapi! Anajua una asset au biashara gani beyond ambavyo alitakiwa akufahamu inaletaga dharau at last. Mie hiki ndio sipendagi
Sasa unavyocheka cheka nao ni lazima watajua unafanya kazi wapi, lazima utaropoka tu mambo yako...badae ndo utajua hujui

Kumsalimiana kunatosha asee[emoji848]
 
Kuogopana ninakozungumzia ndio ile ukikaribisha jirani ataleta wezi,mara utalogwa,wataleta dharau yaani binadamu tunaogopana sana
Lakini kibongo huu ndo ukweli..wezi anakuletea kweli na kukuloga atakuloga oooohoo[emoji849]
 
Sasa unavyocheka cheka nao ni lazima watajua unafanya kazi wapi, lazima utaropoka tu mambo yako...badae ndo utajua hujui

Kumsalimiana kunatosha asee[emoji848]
Hahahah ndio si kutafuta kuonekana jirani mwema tu😅 ! Mie siwezi ila nawashauri wanaoweza tu wafanye hivyo maana dah! Mie naweza kukaa ndani hata siku 2 bila kutoa unyayo nje as long as huduma zote nazipata frijini, jikoni na chooni😅 kukaa vijiweni ni very rare case labda nikakae mbali sana na home! Na ndio maana JF is my first kijiwe
 
Hakuna kurogana so unaweka mipaka binafsi Kuna mmama mmoja nilimkataa live Mana Tabia yake sikupenda. Anaongea majirani walivyo na Tabia zao. Nikajua na huyu namie atawaambia wengine nilivyo. Na ndiye aliyenifanyia usafi wa nyumba wakati nimekamilisha.akataka ukaribu Sana nikamkataa. Saivi nasikia ananisema kuwa natembea na jirani mmoja ivi kisa wakati anafanya usafi aliona Nampa ndio moja ya rangi tupu.yeye aliomba nikamtolea nje nikamwambia ndo naanzia maisha jamani.
Huku hajui huyo mdada yeye aliniokoa na nini
Jirani kukusema kujifanya anakujua kuliko hata unavyojijua hii ndo tabia yao kuu...

Mimi huyu ananitangaza naringa najifanya special siku nikifa ntazikwa na nani khaaaa[emoji848]

Simpendi asee ndo maana mchafu[emoji57]
 
Nadhani watu wengi hawajagundua hili au hawajijui.
Nilichogundua ni watu wengi wabinafsi na wanataka kunyenyekewa.

Mfano wewe unasuffer na roho yako pia kuhangaika kutengeza ujirani na salamu.
Je umejiuliza kwanini wao mpaka leo hii hawajaja kukusalimia?
Kwanini wao ndani ya muda wote wasianze wao uanze wewe?

Majibu yako mengi ila kukusaidia ni labda kwa sababu hawagive a damn about ujirani wala salamu.

Mfano mimi kwenye shida naweza kusaidia mtu yoyote ambaye simjui ila shida ikitokea kwako kwa sababu hawakujui trust me hakuna mtu atakusaidia.

Majirani sio solution ya matatizo unayoyafikiria.
Ni kama Murphy's law.

Murphy's law inamaanisha "anything that can go wrong will go wrong".
Lakini hiyo siyo maana pekee bali pia inamaanisha"chochote kinachoweza kutokea lazima kitatokea" na hutoweza kukizuia.

Strange thing ni watu wengi wanadhani kuwa na majirani ndio itaweza kuprevent bad things au kusaidiwa pale kitu kibaya kitakapotokea, which is wrong and impossible.

Na hiyo inapelekea ile definition ya "Uoga wa Maisha" kuwa applied on this circumstance. It's like the act of seeking security.

Na hiyo ndio sababu kubwa ya watu wengi kutafuta majirani kwa ulazima.
Na wengine wakishauri hivyo kwenye hii thread

Naamini ujirani hauwezi kuwa created deliberately bali ni kama nature's coincidence.
Na kulazimisha itepeleka baadae kukosana au kuonekana mnafiki na kero kwa wengine na hali itakuwa mbaya zaidi.

Personally mtu huyo ningemuona irritative.
Lakini sisi binadamu ni tumetofautiana so it depends.

Sidhani kama umewahi kuishi nje ya africa lakini ungepata tabu kuishi USA sababu asilimia kubwa ya watu ni minding your own business.

Bytheway hiyo ilikuwa opinion yangu even though it's a Fact.
Ukweli mtupu[emoji122]
 
Jirani kukusema kujifanya anakujua kuliko hata unavyojijua hii ndo tabia yao kuu...

Mimi huyu ananitangaza naringa najifanya special siku nikifa ntazikwa na nani khaaaa[emoji848]

Simpendi asee ndo maana mchafu[emoji57]
Umemmaindi sana dah,,, sema ndio hivyo mie mwenyewe nahisi kuna watu watakuwa wanahisi ninaringa ila mie sina habari! Sifa nilionayo tu kitaa wanajua mie sio kicheche 😅😅😅 na kijana mpole sana
 
Unanikumbusha kauli ya mtume muhammad inayosema "lililokupata halikuwa likukose,na ambalo limekukosa halikuwa likupate "

Hiyo law inaendana na maneno ya mtume muhammad kabisa kabisa.

Na ndio naishi katika msingi huoo.

Ilinikamata homa kali sana hakuna jurani ambaye alijua,baada ya kupata afadhali ndo watu wanashangaa nna vidonda mdomoni.

Sihitaji mazoea na watu hata kama nikiumwa.
Huyo Mtume Muhammad unaemsema amehusia Sana watu waishi kwa wema na akazitaja had haki za jirani kwa jirani mwenzake
Kama husalimii majiran na unajitenga nao ww bado humfati Muhammad (S.A.W)
 
Back
Top Bottom