Its Tesha
Senior Member
- Oct 6, 2025
- 168
- 608
Mfanyabiashara Jeniffer Jovin (Niffer) na Mika Chavala @mikachavala ambao wanakabiliwa na mashtaka ya uhaini tayari wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kusikiliza shauri linalowakabili.
Ikumbukwe tarehe 25, Novemba 2025 washtakiwa 20 kati ya 22 ambao walikuwa wanashtakiwa pamoja na Niffer walioachiwa baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka DPP kueleza kuwa hana nia ya kuendelea na mashtaka yao.
Leo pia litaendelea shauri la uhaini dhidi ya Washtakiwa wengine katika mahakama hiyo.