Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Skonzi si ndio buns?
Kama ni hivo basi sawa....
Nakuekea kipimo cha kilo 1...
Mahitaji
Unga kg 1
Samli 8 tablespoon (iyayushe)..
Siagi 5 tablespoon (kwa ladha nzuri zaidi) sio lazima lakini.
Yai 1
Ufuta (sesame seed) kiasi
Chumvi kiasi
Maji
Hamira 1.5 tablespoon
Baking powder 1 teaspoon
Namna ya kutaarsiha
1)Changanya unga wako pamoja na chumvi hamira na baking powder vizuri
2)Weka samli,kiini cha yai na siagi changanya then add maji kidogo kidogo hadi ushikane na kuwa kama wa chapati
3)Kanda vizuri hadi uwe laini...acha for 30 mins uumuke
4) Kata buns zako ukubwa unaohitaji kwa kutengeza shepu duara then panga kwenye trey
5)Chukua brush na pakaa ute juu yake then nyunyizia ufuta...ukimaliza acha hadi yaumuke ndio uweke kwenye oven..
Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
Hapo kwenye kuchanganya na maji pia unaeza weka maziwa badala ya maji