Nifungue kesi gani?

Nifungue kesi gani?

cheguevara

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2012
Posts
1,348
Reaction score
652
Nisaidieni wadau

Gari langu lilikuwa bovu fundi mmoja akasema atalitengeneza kwa laki moja akaja kulitengeneza badae akaanza nunua spare hii mara ile tukakubaliana kuwa nikinua hizo spare gari lisipone utarudisha gharama zangu zote akasema ndiyo, ameninunulisha spare gari halikupona na akakimbia, alikonunua spare inaonekana alinunua kwa bei ya chini kuliko aliyoniambia na kazi hataki kufanya amekuwa akinipiga chenga tu.

Sasa gharama imefikia 5mln na imemshinda akanidanganya atanipa engine ingine lakini wapi na hataki kuchukua spare alizoninunulisha. Je, nimfungulie kesi gani ya kujipatia pesa kwa udanganyifu,wizi wa kuaminiana au madai?

Hapa nafungua kesi gani: Kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, wizi wa kuaminiwa, kesi ya madai au vipi? Naomba msaada wenu wadau?


 
kwanza gari yako ni aina gani, na gharama yake ni Tsh ngapi
 
Huku hakiniusu wengine tunamiliki Helicopter.
 
Jifunze na liwe funzo la mwisho...kupeleka gari lako kwa mafundi uchwara..hao njaa tupu!! tafuta gereji la maana!!
huyo atakupotezea wakati wako,,,,achana nae!!
 
Unachokisema ni tatizo la nchi nzima, mafundi wetu hawana elimu ya ufundi, wengi ni waziba pancha, hawa NIT badala ya kufundisha watu wamekalia kuendesha elimu chonganishi. Hatuna authorized dealers na waliopo wachache kama toyota tanzania wapo kupiga deal za serikali tu, sie nao ni hovyo tu unanunua nissan murano iliyotengenezwa kwa ajili ya nchi za baridi unataka uliendeshe bongo.
 
Pole

Mpaka imefika mil 5 na wewe umo tu.. mmmmh

hii ni kutokana na ukweli kwamba alinihakikishia kuwa litapona na kwamba kama lisingepona angerudisha hizo spare alikonunua nirudishiwe pesa yangu kwa hiyo nlikuwa ananinanunusha spare gari haliponi nikaendelea kumuamini kwamaana kwamba ningerudishwa hela ninunue injini ingine
 
Unachokisema ni tatizo la nchi nzima, mafundi wetu hawana elimu ya ufundi, wengi ni waziba pancha, hawa NIT badala ya kufundisha watu wamekalia kuendesha elimu chonganishi. Hatuna authorized dealers na waliopo wachache kama toyota tanzania wapo kupiga deal za serikali tu, sie nao ni hovyo tu unanunua nissan murano iliyotengenezwa kwa ajili ya nchi za baridi unataka uliendeshe bongo.

Hapo nakuunga mkono mkuu nikweli mafundi wa hapa nchini hawana ujuzi , Nashangaa hata akiziba pacha kwa pikipik anakuomba ufunguo ili a~test kama iko poa.
 
Kama kampuni yake ni kubwa na una uhakika wa kulipwa hela yako bila usumbufu, mfungulie kesi, but kama binafsi huyo fundi ni wa magumashi hiyo hela atakuwa kashatumia hovyo, labda mpe jambajamba anaweza kukulipa hata kwa kuchangiwa na ndugu zake
 
Mkuu kwanza mgonge demand notice afu mpe siku 14 za kukulipa gharama zako,kama vipi ni pm nikucheck jinsi ya kuandika a legal demand notice..!!
 
Fungua case ya civil cause hiyo ni Contractual obligation itakupa uwanja wa kuwa compersated but ya criminal sio rahisi kuwa compersated cause atashitakiwa kwa wizi na unlawful obtaining money..! Under Tort-contractual law unachance ya kuwa recovered your damages
 
Back
Top Bottom