Wanaume wa kiafrika ndoa ya bila mtoto sijui wanaona vipi. Nina rafki yangu toka SriLanka ameolewa na Mduch, hawana mtoto na hawana tatizo lolote. Anasema mumewe hataki watoto kwani wapo watoto kibao wenye shida kwa hiyo wanasubili wife amalize shule wa adopt. Hao wana uwezo wa kuzaa lakini kimtazamo wao mtoto si lazima umzae waweza kulea wale wasio na walezi. Laiti familia zenye matatizo ya uzazi zingefanya kama hawa ndugu, kuliko kuleta mawazo kwa wake zao na kuhatarisha maisha yao.
Kimada ni obvious akijua mkeo hazai lazima ajilengeshe au hata akubambikie mimba. Na am sure hataweza kumheshimu mkeo kwani atamuona mgumba yeye ndio kila kitu kwa kuwa kazaa. Na mindugu ya kiafrika navyoijua ndio mama we; huyo ndio atakuwa mkwe rasmi; kaleta mtoto!