Sikitika sababu unapooa sio kwamba unaoa ili uzae bali uishi na mpenzi wako mpaka mwisho wa maisha yenu, Unapozaa nje kwanza unakuwa umevunja agano na Mungu pi na mwenza wako, kumbuka uliapa mbele za mwenyezi Mungu mtavumiliana kwa shida na raha iweje leo unaenda kuzaa na msichana mwingine? unajuaje kama hajakuchakachua labda ni wewe mwenye matatizo? Unajuaje kwamba wewe sio mwanzo wa matatizo kwamba mkeo hapati ujauzito?
Maana wababa wakishakuwa na vimada wanajikuta wanafanya mapenzi na wake zao mara moja kwa mwezi, unajuaje kwamba huo ndio muda wake wa kupata ujauzito?Kwa kweli sikitika sababu ulichofanya sio halali kabisa......