Niger ni kipimo kingine cha ujinga wa binadamu

lee Vladimir cleef

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
9,571
Reaction score
35,475
Vita huja kwa ajili ya kuokoa wengi wasijeumizwa na wengine,majeshi yapo kwa ajili ya ulinzi wa mataifa Yao ili yasivamiwe na wakorodi.

Ingawa Ni kweli, toka zamani vita zilitumika kuleta usawa pasipokua na usawa,kuleta haki pasipokua na haki,lkn ni vema kutatmini madhara na faida ya vita kabla ya kuanzisha vita.

Niger kunaweza kupelekea kutokea vita kubwa sana kwa Afrika yetiu amabayo haikuwahi kutokea toka kuumbwa kwa Dunia hii.

Vita hii inaweza kua kubwa zaidi kushinda hata vita baina ya Urusi na NATO huko Ukraine kwa Sasa, kwa sababu huko ni Urusi dhidi ya NATO kwa kuwatumia Ukraine,wakati Huku ni pande mbili, upande mmoja una nchi baadhi ya ECOWAS zikiongozwa na Nigeria na zikiungwa mkona na NATO.

Ingawa hapa ni USA na France, lkn mambo yakianza UK na akina German watasidia kwa namna moja ama nyingine.

Upande wa pili Kuna Niger Bukinafaso,Mali na washirika wake, hawa wakitetewa na Urusi.

Hawa pia mambo yakiwa magumu Kuna akina china na wenzao watasaidia kwa namna moja ama nyingine.
Hata hivyo pande zote mbili Zina waungaji wengine mikono ambao bado wako kimya ila mambo yakiharibika watajitikeza zaidi.

Kama vita ikianza itachukua mkondo wa kidunia zaidi badala ya kikanda,kwa sababu tayari wakingia vifua Wana chuki zao za asili na hata sasa huko Ukraine wanaendela kufanyiana unyama, yaani West na East. Kibaya zaidi vita hii pia Ina chembe ya madhara ya vita vya Ukraine, kwani west wameiwekea vikwazo Urusi na wanataka wasinunue gesi yake Ili Urusi ifilisike, nayo Urusi imeamua kupiga fitina ili wasipate gesi sehemu nyingine ili nao west wafilisike.yaani wangeweza kupata gesi toka Nigeria, kupitia Niger hadi urope.

Sasa hapa ujinga uko hivi. Ecowas wanataka kumrudisha madarakani mtu mmoja TU aliepinduliwa,kwa kuwatoa wapindua nchi wanaweza kuwa kumi tu. Lakini mwisho wa siku itatokea watakufa watuwatakufa watu milioni kumi. Je, huu sii ujinga wa ECOWAS.

Je, ECOWAS wamejaribu njia za diplomasia?

Ecowas wanafuata tqbia zilezile za USA,kutatua matatizo kama hayo kwa njia za vita,na mwisho wake hufa watu Kwa mamilioni.

Mfano Iraq Inamiliki WMD ipigwe, kiduku anamuliki nuke apigwe, hebu fikiria hapa mziki wake wangekufa wangapi? Gadafi mkorofi apigwe. Hatumpendi Assad wa Syria apigwe. Ecowas wanataka kutupeleka Huku kichwakichwa.

Narudia Tena ili kumrudisha mtu mmoja tu inabidi ecowas iwatoe madarakani wanamapinduzi kumi kwa mfano wa Niger, na ili kuwaondoa watu hao kumi ,basi ecowas wajiandae kupoteza wanadamu wasiopungua million kumi.

Maana watakufa wanajeshi na wasio wanajeshi,wa ECOWAS na Niger na WA nchi zisizo katika mgogoro huu.
watakufa watu kwa risasi mabomu na njaa.

Kumrudisha mtu mmoja tutarajie watu miion kumi. Hapa ndio Pana ujinga wa mwanadamu.
 
Urusi itaunga mkono nchi yoyote ambayo inataka kutetea masilahi yake ya kitaifa dhidi ya Magharibi." - Vladmir Putin.

Katikq kongamano la Jeshi la 2023, rais wa Urusi, Vladmir Putin asema kuwa Moscow iko wazi kwa ushirikiano sawa wa kiulinzi na mataifa yote yanayotaka kulinda masilahi yao.

Maneno yake halisi: "Urusi iko tayari kuzidisha ushirikiano sawa wa kiteknolojia na ushirikiano wa kiulinzi na nchi zingine, i.e. wale wote wanaotaka kulinda masilahi yao ya kitaifa na njia huru ya maendeleo, na wanaamini ni muhimu kufanya juhudi za pamoja za kujenga mfumo wa usawa na usalama usiogawanyika ambao ungelinda kila nchi kwa uhakika,”
 
Vita huja kwa ajili ya kuokoa wengi wasijeumizwa na wengine,majeshi yapo kwa ajili ya ulinzi wa mataifa Yao ili yasivamiwe na wakorodi.

Ingawa Ni kweli, toka zamani vita zilitumika kuleta usawa pasipokua na usawa,kuleta haki pasipokua na haki,lkn ni vema kutatmini madhara na faida ya vita kabla ya kuanzisha vita.

Niger kunaweza kupelekea kutokea vita kubwa sana kwa Afrika yetiu amabayo haikuwahi kutokea toka kuumbwa kwa Dunia hii.

Vita hii inaweza kua kubwa zaidi kushinda hata vita baina ya Urusi na NATO huko Ukraine kwa Sasa, kwa sababu huko ni Urusi dhidi ya NATO kwa kuwatumia Ukraine,wakati Huku ni pande mbili, upande mmoja una nchi baadhi ya ECOWAS zikiongozwa na Nigeria na zikiungwa mkona na NATO.

Ingawa hapa ni USA na France, lkn mambo yakianza UK na akina German watasidia kwa namna moja ama nyingine.

Upande wa pili Kuna Niger Bukinafaso,Mali na washirika wake, hawa wakitetewa na Urusi.

Hawa pia mambo yakiwa magumu Kuna akina china na wenzao watasaidia kwa namna moja ama nyingine.
Hata hivyo pande zote mbili Zina waungaji wengine mikono ambao bado wako kimya ila mambo yakiharibika watajitikeza zaidi.

Kama vita ikianza itachukua mkondo wa kidunia zaidi badala ya kikanda,kwa sababu tayari wakingia vifua Wana chuki zao za asili na hata sasa huko Ukraine wanaendela kufanyiana unyama, yaani West na East. Kibaya zaidi vita hii pia Ina chembe ya madhara ya vita vya Ukraine, kwani west wameiwekea vikwazo Urusi na wanataka wasinunue gesi yake Ili Urusi ifilisike, nayo Urusi imeamua kupiga fitina ili wasipate gesi sehemu nyingine ili nao west wafilisike.yaani wangeweza kupata gesi toka Nigeria, kupitia Niger hadi urope.

Sasa hapa ujinga uko hivi. Ecowas wanataka kumrudisha madarakani mtu mmoja TU aliepinduliwa,kwa kuwatoa wapindua nchi wanaweza kuwa kumi tu. Lakini mwisho wa siku itatokea watakufa watuwatakufa watu milioni kumi. Je, huu sii ujinga wa ECOWAS.

Je, ECOWAS wamejaribu njia za diplomasia?

Ecowas wanafuata tqbia zilezile za USA,kutatua matatizo kama hayo kwa njia za vita,na mwisho wake hufa watu Kwa mamilioni.

Mfano Iraq Inamiliki WMD ipigwe, kiduku anamuliki nuke apigwe, hebu fikiria hapa mziki wake wangekufa wangapi? Gadafi mkorofi apigwe. Hatumpendi Assad wa Syria apigwe. Ecowas wanataka kutupeleka Huku kichwakichwa.

Narudia Tena ili kumrudisha mtu mmoja tu inabidi ecowas iwatoe madarakani wanamapinduzi kumi kwa mfano wa Niger, na ili kuwaondoa watu hao kumi ,basi ecowas wajiandae kupoteza wanadamu wasiopungua million kumi.

Maana watakufa wanajeshi na wasio wanajeshi,wa ECOWAS na Niger na WA nchi zisizo katika mgogoro huu.
watakufa watu kwa risasi mabomu na njaa.

Kumrudisha mtu mmoja tutarajie watu miion kumi. Hapa ndio Pana ujinga wa mwanadamu.
Hao wahuni sio wa kuchekewa, lazima washurutishwe kuurejesha utawala wa kidemokrasia wa Bazoum.
 
UK iliongozwa na kile kibibi karbu miaka 70 saiv mwanae nae anakula mema tu alafu huyo mtu anakuja kukuambia lazima tufuate democrasia aseee aliyeturoga alegezee kidogo kama amekufa huyo mwenye mikoba atuague bhasi
 
Hii vita ikianza na Nigeria ikishiriki basi naye inawezekana kwake pia kunaweza waka moto kwa sababu wale wa Biafra bado wana ndoto ya kujitenga
Na miye nitawaunga mkono Biafra
UK iliongozwa na kile kibibi karbu miaka 70 saiv mwanae nae anakula mema tu alafu huyo mtu anakuja kukuambia lazima tufuate democrasia aseee aliyeturoga alegezee kidogo kama amekufa huyo mwenye mikoba atuague bhasi
Aahaàaaa
 
Kama Raisi alikuwa anaiendesha nchi vibaya na haonyeki basi ni sahihi tu kupinduliwa.

Hao ECOWAS na US watakuwa na interest zao tu
 
Wanamapinduzi wa Niger wanamtaji wa kumshikilia kibaraka wa Weast huku nao wamepiga biti uvamizi wowote wa kijeshi nchini Niger ni kuhatarisha uhai wa raisi waliyemateka.
 
Kwanini mnatetea Sana tawala za kijeshi? Wanajeshi wa Niger hawataki tawala za democracy tokea uhuru wamepindua mara 8
Kwan wananchi waniger wameomba msaada kuondoa huo utawala wa kijeshi?!
 
Toka dunia iumbwe, lugha anayoelewa binadamu ni ubabe na vita. Kwa maelfu ya miaka mwenye nguvu ndiye anatawala. Hata leo anayetawala dunia ni mwenye nguvu. Habari za utawala wa kiraia na kidemkokrasia ni uongo tu.
 
Back
Top Bottom