Nigeria :Aliyefungwa Kwa Kubaka Hana Hatia

Dalton Elijah

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2022
Posts
968
Reaction score
1,978
Baada ya kukaa jela kwa miaka minane mwinjilisti kutoka Nigeria anayetuhumiwa kuwabaka wasichana wa kanisa lake la Afrika Kusini amepatikana hana hatia kwa mashtaka yote.

Timothy Omotoso alikuwa amekanusha mashtaka 32 katika kesi iliyorushwa moja kwa moja na kufuatiliwa kwa kiasi kikubwa Afrika ya Kusini. Mnamo mwaka wa 2018, shahidi mmoja aliiambia mahakama kwamba alibakwa na kasisi huyo, ambaye alikuwa akiongoza kanisa katika jiji la Port Elizabeth, alipokuwa na umri wa miaka 14.

Akitoa uamuzi huo Jumatano, hakimu aliyesimamia kesi hiyo alisema kuwa Bw Omotoso amepatikana hana hatia kwa sababu waendesha mashtaka waliiendesha vibaya kesi hiyo.

Mamlaka ya Kitaifa ya Mashtaka ya Afrika Kusini (NPA) ilitoa tathmini sawa na hiyo, ikisema kwamba "waendesha mashtaka wa zamani katika kesi hiyo walifanya isivyofaa na washtakiwa hawakuhojiwa vya kutosha na serikali".

NPA ilisema sasa "itazingatia sheria" na kwamba hali ya kutokamilika kwa kesi hiyo ilitokana na Bw Omotoso kuwasilisha changamoto nyingi za kisheria. #EastAfricaTV
 
Rupia imeshapenyezwa au mkakati umeshatik.
 
Hakuna nchi ya hovyo kama Nigeria. Kila kitu kinawezekana.
 
Back
Top Bottom