Nigeria ilianza kuchimba mafuta 1956, bado inauza mafuta ghafi nje na kununua yaliyosafishwa. Tanzania tutatoboa na gesi?

Sera ya mabeberu ni kutufanya tuwewazalishaji wa malighafi tu.

To never produce anything.

Wanatulazimisha mikopo kwa fedha zao na wanatupangia bei ya mauzo ya raw materials.
Hao mabeberu wapo Africa pekee hayo mabara mengine mabeberu wapo likizo?
 
Hapo kuna, wanaigeria, tena viongozi wananufsika na huo uozo, ili nchi ya Afrika, inufaike na rasilimali zake,lazima uanzishe Vita na UK, ulaya, America, maana Hawa wajomba hawapo tayari kuona Rasilimali zinanufsisha wazawa, wataua, watatoa rushwa,watawakamata makenge watatu wa kiafrika,wawape mpunga, na Hao watauza nchi,
Mkapa alijiuzia mgodi!kikwete aliuza gesi yetu kwa wanzungu, Ukitqka Uwe kama Iran, south Afrika, au, china, lazima ujipange kupambana na mabepari!
Kama hivyo bora ya ukoloni maisha yalikuwa nafuu kwa mwafrika kuliko baada ya Uhuru ni tabu tupu
 
Hao mabeberu wapo Africa pekee hayo mabara mengine mabeberu wapo likizo?

Hoja ya msingi sema haya mataifa yakishindwa, yanapeleka vita, wakishindwa kuwachonganisha wanafika wenyewe..
 
Nchi za magharibi zina nguvu sana hasa katika kuendesha masoko ya kimataifa.

Hapo kiwanja cha Julius Nyerere Int. Airport: Wazungu walikataa kuwa kiwanja hakina hadhi ya kuwa airport ya kimataifa kwa sababu hakina magari ya zimamoto. Kumbuka walimkatalia Nyerere kumuuzia hizo gari za zimamoto.

Nyerere akajimwambafai ajitoe kwenye hiyo matrix, akaunda magari ya zimamoto (nafikiri ndio hiyo nyumbu kwa sasa). Walivyoona anapandisha mabega wakaamua kumpatia sasa hizo gari za zimamoto asije akaanza kujitegemea.

Kiufupi nchi yoyote ya kiafrika ikitaka ijitegemee kwa kilaa kitu lazima itakutana na upinzani mkubwa wa hali ya juu.

Pia na system yetu tuliyoachiwa na wazungu ni ngumu sana kutoboa.

Mfano:
Mtu kakamatwa na bunduki ya kutengeneza kwa mkono, akikamatwa mtu huyu ataishia kufungwa tu badala ya kumchukua na kuendeleza hiki kipaji, pengine anaweza akawa asset kwa taifa.

Au
Ajitokeze mtu avumbue dawa ya UKIMWI au Kansa, mtu wa hivi ngumu kumaliza mwaka kuna uwezekano mkubwa wakalala nae mbele.
Swali zuri sana. Tuna akili kama waarabu kuchukua kila kitu 50/50, no 51/49 kwenye makubaliano tuwe na sauti kubwa baada ya miaka 10 vyote viwe vyetu.
 
Nigeria ni nchi ya pili kwa uzalishaji mafuta barani nyuma ya Angola, ilianza rasmi uchimbaji mafuta na kuyauza nje kibiashara mwaka 1956, kufikia mwaka 2000 mapato ya mafuta ghafi yalikuwa 98% ya mapato yote Nigeria iliyopata kwa kuuza bidhaa na huduma nje ya nchi.

Pamoja na mafuta ghafi kuwa chanzo kikuu cha mapato ya fedha za kigeni Nigeria bado iliingia gharama kubwa kuagiza mafuta yaliyosafishwa kwa miaka yote.

Kiwanda cha Dangote kimeanza rasmi uzalishaji lakini bado kina safari kuelekea kuzalisha kwenye uwezo wake unaotarajiwa ili kutosheleza mahitaji ya ndani.

Ni safari ya zaidi ya miaka 68 kwa nchi hii iliyo magharibi mwa Afrika, tutegemee safari hii kwa gesi yetu kuweza kuifanya kimiminika(LPG) ili iweze kutumiwa kwa matumizi mbalimbali? Tanzania tunanunua gesi ya kupikia inayojazwa kwenye mitungi kwasababu tumeshindwa kuweka mitambo ya kuifanya LPG huku yetu tukiiuza nje!

Nchi za kiarabu ziliwezaje kutumia mafuta yake mapema na kuwatoa kwenye lindi la umasikini kufikia utajiri wa kiwango cha juu!
Wapumbavu sana viongozi wetu wote.

Ilitakuwa iwe kama USA kama wangekuwa na akili.
 
Kula uliwe.

Hapo ndipo uelewe hakuna nchi ya magharibi inayokutakia mema.

Mwendazake alizuwia mradi mkubwa wa kuifanya gas yetu itumiwe na wote na itowe gas nyingine za ziyada. Mpaka leo sielewi kwanini alifanya hivvyo. labda alifikiri itakuwa ni wepesi tu lufanya sisi wenyewe kama vile kufanya kwenye maabara? Sielewi kwanini, au ndiyo alijimwambafai kukataa kula uliwe?

Waarabu walibali mapema sana kula uliwe, ndiyo maana hawakauwa na matatizo makubwa, wameenda nao wababe taratibu mpaka leo hii. Wakijidai kugoma kuliwa itakula kwao kimoja.

Dangote kishaunda refinery kiubwa sana Nigeria kuitumia fursa, sielei kama imeshaanza kutumika au vipi.

Kuhusu Taanzania, siyo Gas pekee tuliyonayo, hata mafuta tunayo lakini tukijitia wajanja hatutaichimba.
 
Hapo kuna, wanaigeria, tena viongozi wananufsika na huo uozo, ili nchi ya Afrika, inufaike na rasilimali zake,lazima uanzishe Vita na UK, ulaya, America, maana Hawa wajomba hawapo tayari kuona Rasilimali zinanufsisha wazawa, wataua, watatoa rushwa,watawakamata makenge watatu wa kiafrika,wawape mpunga, na Hao watauza nchi,
Mkapa alijiuzia mgodi!kikwete aliuza gesi yetu kwa wanzungu, Ukitqka Uwe kama Iran, south Afrika, au, china, lazima ujipange kupambana na mabepari!

Shida ya Africa ni Waafrica siku zote, hata zama za utumwa mzungu au muarabu hakuja na mshua akaanza kubeba watumwa ila alitumia waafrika kuwauza waaafrika wenzao

Na hata sasa hakuna mzungu anaekuja afrika na kuinunua Afrika kwa bei anayoitaka pasipo dalali wa kiafrika.

Hivyo, adui wa Afrika yupo Afrika
 
Kula uliwe.

Hapo ndipo uelewe hakuna nchi ya magharibi inayokutakia mema.

Mwendazake alizuwia mradi mkubwa wa kuifanya gas yetu itumiwe na wote na itowe gas nyingine za ziyada. Mpaka leo sielewi kwanini alifanya hivvyo. labda alifikiri itakuwa ni wepesi tu lufanya sisi wenyewe kama vile kufanya kwenye maabara? Sielewi kwanini, au ndiyo alijimwambafai kukataa kula uliwe?

Waarabu walibali mapema sana kula uliwe, ndiyo maana hawakauwa na matatizo makubwa, wameenda nao wababe taratibu mpaka leo hii. Wakijidai kugoma kuliwa itakula kwao kimoja.

Dangote kishaunda refinery kiubwa sana Nigeria kuitumia fursa, sielei kama imeshaanza kutumika au vipi.

Kuhusu Taanzania, siyo Gas pekee tuliyonayo, hata mafuta tunayo lakini tukijitia wajanja hatutaichimba.

Ujanja upi wa kula uliwe uliowahi kufanikiwa nchini

Huo wa Mwadui, Geita na Mererani ambao hata impact yake haijulikani ni nini maana umaskini wa hayo maeneo hauakisi utajiri uliokuwepo kwenye ardhi.

Nitamlaumu Magufuli kwa mengi ila kwenye madini, alipaswa hufanya hesitations alizofanya na hiyo helium itachimbwa na umaskini utaendelea. Tupo hapa
 
Ujanja upi wa kula uliwe uliowahi kufanikiwa nchini

Huo wa mwadui, geita na mererani ambao hata impact yake haijulikani ni nini maana umaskini wa hayo maeneo hauakisi utajiri uliokuwepo kwenye ardhi.

Nitamlaumu Magufuli kwa mengi ila kwenye madini, alipaswa hufanya hesitations alizofanya na hiyo helium itachimbwa na umaskini utaendelea. Tupo hapa
Zako kama hujuwi zinakwenda wapi, tazama panya labda wanazila.

Hujasikia kuwa ujinga wetu ni tunaiibia Tanzania halafu pesa tunakwenda kuiweka hukohuko kwa wajanja.

Jikumbushe, bofya link chini hapo:

Nigeria ni nchi ya pili kwa uzalishaji mafuta barani nyuma ya Angola, ilianza rasmi uchimbaji mafuta na kuyauza nje kibiashara mwaka 1956, kufikia mwaka 2000 mapato ya mafuta ghafi yalikuwa 98% ya mapato yote Nigeria iliyopata kwa kuuza bidhaa na huduma nje ya nchi.

Pamoja na mafuta ghafi kuwa chanzo kikuu cha mapato ya fedha za kigeni Nigeria bado iliingia gharama kubwa kuagiza mafuta yaliyosafishwa kwa miaka yote.

Kiwanda cha Dangote kimeanza rasmi uzalishaji lakini bado kina safari kuelekea kuzalisha kwenye uwezo wake unaotarajiwa ili kutosheleza mahitaji ya ndani.

Ni safari ya zaidi ya miaka 68 kwa nchi hii iliyo magharibi mwa Afrika, tutegemee safari hii kwa gesi yetu kuweza kuifanya kimiminika(LPG) ili iweze kutumiwa kwa matumizi mbalimbali? Tanzania tunanunua gesi ya kupikia inayojazwa kwenye mitungi kwasababu tumeshindwa kuweka mitambo ya kuifanya LPG huku yetu tukiiuza nje!

Nchi za kiarabu ziliwezaje kutumia mafuta yake mapema na kuwatoa kwenye lindi la umasikini kufikia utajiri wa kiwango cha juu!
Mkuu wangu hongera sana kwa bandiko zuri lililojaa hoja zenye mantiki.

Nikianza na hoja ya msingi, kinachofanya Nigeria washindwe kuyachakata mafuta yao kwaajili ya matumizi ya ndani nisababu za kisera na mikataba ya mafuta waliyoingia.

Wakati mwingine wawekezaji hutazama palipo na soko kubwa. Wawekezaji huhitaji kurudisha gharama zao za uwekezaji mapema ndio sababu huchagua kuuza mafuta ghafi kwa mataifa ya nje yenye viwanda vyakuyachakata.

Mbali na hivyo makampuni huogopa gharama za kujenga viwanda vya uchakataji wakati mwingine kwasababu ya ukosefu wa mtaji. Hapa tunazungumzia mwekezaji amewekeza trillioni za pesa kwenye utafutaji, uchimbaji na uzalishaji unamwambia atafute pesa zingine awekeze kwenye kiwanda cha uchakataji. Hapo kuna uwezekano mkubwa akachagua kuuza mafuta ghafi kwenye mataifa ya nje.

Kwa upande wa kutumia gesi iliyogunduliwa Tanzania majumbani tayari serikali ilishaanza kutandaza mabomba ya kupitisha gesi majumbani. Bomba la gesi linafika mpaka jikoni kwako.

Gesi iliyogunduliwa Tanzania ni Methane. Moja ya sifa ya hiyo gesi huwezi ijaza kwenye mtungi ili uitumie kupikia ikiwa kwenye mtungi.

Hivyo mkuu ni tofauti kabisa na LPG, gesi zilizopo kwenye LPG ni butane na propane, ambazo hazipo kwenye gesi iliyogunduliwa Tanzania.

Na mpaka muda huu wapo watanzania wachache wazalendo walishaanza kutumia gesi iliyogunduliwa Tanzania kwenye magari yao. Kama una gari yako ibadilishe ili iweze kutumia gesi. Na vituo vya kujaza gesi tayari vipo Dar es Salaam.

Mwisho kabisa kama kweli una lengo la kutumia gesi iliyogunduliwa Tanzania ni vyema ukafika TPDC ili wakupe utaratibu wa kukusogezea bomba la gesi nyumbani kwako.

Kumbe basi Tanzania sio kama Nigeria. Tanzania ni yetu sote, tuna enjoy rasilimali zetu.
 
Mkuu wangu hongera sana kwa bandiko zuri lililojaa hoja zenye mantiki.

Nikianza na hoja ya msingi, kinachofanya Nigeria washindwe kuyachakata mafuta yao kwaajili ya matumizi ya ndani nisababu za kisela na mikataba ya mafuta waliyoingia.

Wakati mwingine wawekezaji hutazama palipo na soko kubwa. Wawekezaji huhitaji kurudisha gharama zao za uwekezaji mapema ndio sababu huchagua kuuza mafuta ghafi kwa mataifa ya nje yenye viwanda vyakuyachakata.

Mbali na hivyo makampuni huogopa gharama za kujenga viwanda vya uchakataji wakati mwingine kwasababu ya ukosefu wa mtaji. Hapa tunazungumzia mwekezaji amewekeza trillioni za pesa kwenye utafutaji, uchimbaji na uzalishaji unamwambia atafute pesa zingine awekeze kwenye kiwanda cha uchakataji. Hapo kuna uwezekano mkubwa akachagua kuuza mafuta ghafi kwenye mataifa ya nje.

Kwa upande wa kutumia gesi iliyogunduliwa Tanzania majumbani tayari serikali ilishaanza kutandaza mabomba ya kupitisha gesi majumbani. Bomba la gesi linafika mpaka jikoni kwako.

Gesi iliyogunduliwa Tanzania ni Methane. Moja ya sifa ya hiyo gesi huwezi ijaza kwenye mtungi ili uitumie kupikia ikiwa kwenye mtungi.

Hivyo mkuu ni tofauti kabisa na LPG, gesi zilizopo kwenye LPG ni butane na propane, ambazo hazipo kwenye gesi iliyogunduliwa Tanzania.

Na mpaka muda huu wapo watanzania wachache wazalendo walishaanza kutumia gesi iliyogunduliwa Tanzania kwenye magari yao. Kama una gari yako ibadilishe ili iweze kutumia gesi. Na vituo vya kujaza gesi tayari vipo Dar es Salaam.

Mwisho kabisa kama kweli una lengo la kutumia gesi iliyogunduliwa Tanzania ni vyema ukafika TPDC ili wakupe utaratibu wa kukusogezea bomba la gesi nyumbani kwako.

Kumbe basi Tanzania sio kama Nigeria. Tanzania ni yetu sote, tuna enjoy rasilimali zetu.
Asante kwa pongezi ndugu meneja,
Nakumbuka Tanzania ina mkataba wa Tangu 2022 na wawekezaji kuibadili gesi asilia kuwa CNG wenye thamani ya zaidi ya trilioni 70.

Screenshots_2024-01-18-18-04-09.png

Kuhusu kutandaza mabomba, changamoto watakayokutana nayo ni mipango miji, haitaweza kufika maeneo mengi ndio maana mpaka sasa imeweza kufika Oysterbay na maeneo machache kama hayo.
 
Kuchimba mafuta,gesi,na madini muhimu Africa na kuyachakata kwa kiwangi cha matumizi inawezekana kabisa.

Yazingatiwe haya.
(1) Viongozi wa kiafrika na wananchi kwa ujumla waondokane na ubinafsi na kuukaribisha uzalendo wa kweli na si wamdomoni.
(2) Waafrika wote tuwe na umoja wa kweli ili kujenga uwanda mpana wa soko la bidhaa zetu ,hapa wazungu wataona hakuna namna lazima wakuvaliane na sera za Afrika.
(3) Taasisi za kiafrika zinazo jihusisha na uvumbuzi wa technology na utaalamu mbalimbali zipewe nguvu za kujiendesha bila kuteteleka na kuogopa.
(4) Viongozi wa wasijipendekeze kwa wazungu kana kwamba hawawezi bila wazungu . Tuondoe woga mbele ya wazungu na tusionyeshe kuwaponda na kushindana nao ,yaani tuwe na mifumo inayo jilinda na kulinda usalama wa taasisi zetu.
(5) Tuweke sheria za wawekezaji kujenga viwanda hapahapa afrika badala ya kuchukuwa maligafi na kupeleka kwao. Na hapa ndipo tunapo ibiwa sana.

(6) Tuluhusu watu wetu kupata mitaji na ku support kwa kila hali ili kufikia ushindani wa kimataifa ,tuwajenge akina Dangote wengi afrika.

Wazungu wametuibia na kutunyonya sana ,si tu kwasababu wana akili nyingi ,bali sisi wenyewe tumewapa mwanya huo wa kutuibia .

Kwamfano leo nasikia kuwa Kampuni moja iliyo kuwa inachimba madini ya kutengenezea betri huko Ruvuma ,Imegundua kuwa eneo hilo lina madini mengine mengi aina ya dhahabu,alumasi ,nk .

Kwa hali ya kawaida mpaka wameamua kusema kuwa kuna madini tunadhani wamesha kwapua kiasi gani mpaka wakaona waiambie serikali uwepo wa madini hayo???

Wazungu ni wajanja na wanavifaa vyenye technology ya hali ya ju ,kwahiyo wanapo sema wanataka kuwekeza mahali ,wanakuwa tayari wanamalengo zaidi ya hilo wanalo wekeza kwalo .

Sisi tunakuwa busy na kugombania vyeo vya kisiasa ,mara chama tawala na wapinzani.

MWAFRIKA SHITUKA
 
Nchi za magharibi zina nguvu sana hasa katika kuendesha masoko ya kimataifa.

Hapo kiwanja cha Julius Nyerere Int. Airport: Wazungu walikataa kuwa kiwanja hakina hadhi ya kuwa airport ya kimataifa kwa sababu hakina magari ya zimamoto. Kumbuka walimkatalia Nyerere kumuuzia hizo gari za zimamoto.

Nyerere akajimwambafai ajitoe kwenye hiyo matrix, akaunda magari ya zimamoto (nafikiri ndio hiyo nyumbu kwa sasa). Walivyoona anapandisha mabega wakaamua kumpatia sasa hizo gari za zimamoto asije akaanza kujitegemea.

Kiufupi nchi yoyote ya kiafrika ikitaka ijitegemee kwa kilaa kitu lazima itakutana na upinzani mkubwa wa hali ya juu.

Pia na system yetu tuliyoachiwa na wazungu ni ngumu sana kutoboa.

Mfano:
Mtu kakamatwa na bunduki ya kutengeneza kwa mkono, akikamatwa mtu huyu ataishia kufungwa tu badala ya kumchukua na kuendeleza hiki kipaji, pengine anaweza akawa asset kwa taifa.

Au
Ajitokeze mtu avumbue dawa ya UKIMWI au Kansa, mtu wa hivi ngumu kumaliza mwaka kuna uwezekano mkubwa wakalala nae mbele.
Sijui nani aliwaaminisha watanzania kua ukivumbua kitu una fungwa/Kupotezwa naonaga ni story za vijiweni.

Sent from my CPH1819 using JamiiForums mobile app
 
Utajiri wa Angola nusu umeishia kwa raisi wa nchi hio kupitia binti yake kama mwanamke tajiri kuliko wote Africa,mapato ya Nigeria yameishia kunufaisha mafisadi wakubwa wa nchi hio ambao wengi ni viongozi huku mamilioni wakitopea kwenye umasikini mkubwa.
Utajiri wa Afrika kwa ujumla wake umeishia kuwanufaisha wageni. Hao uliowataja wanapata makombo tu.
Sababu kubwa ya utajiri huo kuchukuliwa ni fikra mbaya za wananchi na viongozi (ujinga na ubinafsi wa kipumbavu).
Hata hivyo, viongozi wapumbavu hutokana na wananchi wapumbavu.
Pamoja na utandawazi wote bado leo wageni wanapewa maliasili, njia kuu za uchumi na kandarasi zote kubwa?
Fikra zinaboreka au zinadumaa?
Kusoma na kuwa na akili ni vitu viwili tofauti, Ila kwa wapumbavu ni kimoja.
 
Shida ya mzawa nae ukimpa kandarasani anagawa nusu anaweka mfukoni mwake kununulia mabus,malori na kuhonga wanawake wote weupe mjini anataka wawe wake.
Nusu iliyobakia wanagawana hakimu,mkurugenzi,mkuu wa wilaya,waziri,meneja,hajali kuhusu mwananchi
 
Huu ndiyo huo ubinafsi wa kipumbavu nilioutaja.
Mkandarasi anapata faida ya moja kwa moja kifedha katika mradi huo.
Hivyo anatakiwa afanye kwa ufanisi ili apewe miradi mingine faida ziongezeke.
Miradi ikikamilika kama ilivyokusudiwa ni faida kwa wananchi na taifa kwa ujumla.
Hivyo hao makandarasi wanaogawana pesa na viongozi ni maadui wa taifa na kazi za usalama wa taifa ni pamoja na kuwashughulikia watu hawa.
Hata hivyo, kama watagawana faida halali siyo shida kubwa ikiwa miradi itakamilika kwa ubora uliokisudiwa na hawakuiba pesa ya uma.
 
Back
Top Bottom