Nigeria: Kijana wa miaka 17 ashikiliwa kwa kuwapa mimba wanawake 10

Nigeria: Kijana wa miaka 17 ashikiliwa kwa kuwapa mimba wanawake 10

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Jeshi la Polisi la Jimbo la Rivers Nigeria limemkamata mvulana mwenye umri wa miaka 17 aliyetambulika kwa jina la Noble Uzuchi na Chigozie Ogbonna (29) kwa madai ya kuwapa ujauzito wanawake 10 kwa ajili ya biashara haramu ya kuuza watoto.

Waliokamatwa wengine ni washukiwa wawili wa kike, Favour Bright (30) na Peace Alikoi (40) ambao wamedaiwa kuendesha kiwanda cha watoto katika maeneo ya Obio/Akpor na Ikwerre katika jimbo hilo.

Imeeleza kuwa Uzuchi na Ogbonna walikodiwa ili kufanya mapenzi na wasichana hao na kuwapa ujauzito.

Msimamizi wa Polisi, Iringe-Koko amesema kwamba uchunguzi uligundua kuwa mwathirika anapojifungua, mtoto walimhifadhi na kumlipa mama kiasi cha N500,000 [TZS milioni 2.5] na kwamba baadhi ya watoto waliojifungua awali walikuwa wameuzwa tayari.

Waathiriwa wote walikiri kwamba walishawishiwa kwa uuzaji haramu wa watoto kwa sababu ya hitaji la kukabiliana na changamoto za kifedha,” ameeleza.

Aidha, Askari wa Kitengo cha Ujasusi walivamia nyumba mbili, ambapo wahanga wa biashara ya watoto walikuwa wakihifadhiwa na kufanikiwa kuwaokoa wanawake hao.
 
Kuna documentary ya bbc nliangalia i thnk kenya, na penyewe kulikua na huo mchezo sana.
Wanaiba watoto wanenda kuwauza hasahasa kwa wale wanawake ambao wameshindwa kupata watoto na ndoa hazipo murua.
Lakini huko nigeria nahs ni mambo yao ya kupigana vata
 
Mambo mengine ni magumu hata kuyafikiria unashindwa.
 
Back
Top Bottom