Nigeria: Msanii agoma kumsapoti mwanasiasa kwenye kampeni ili heshima yake kwa kila mtu ibaki palepale

Nigeria: Msanii agoma kumsapoti mwanasiasa kwenye kampeni ili heshima yake kwa kila mtu ibaki palepale

Mung Chris

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2017
Posts
3,391
Reaction score
3,849
Msanii maarufu nchini Nigeria na mchezaji wa filamu Nollyhood amekataa kiasi cha Naira 10,000,000 sawa na shillingi 54,935,758.91 za Tanzania ili kumsapoti mwanasiasa anayefanya kampeni, mwanasiasa huyo aliona akimtumia huyo msanii kwenye kampeni atapata wanachama wengi na kura zitaongezeka, ila msanii huyo aliona hawezi kujichanganya,

Hivyo kuwaacha wafuasi wake waamue watakavyo maana kila mtu ana mapenzi na anayemuona anamfaa, yote hayo ni pamoja na kulinda heshima yake kwenye tasnia na ili awe wa yeyote yule atakaye ipenda kazi yake haijalishi chama, dini kabila na uraia.

Screenshot_20220802-085359_Twitter.jpg
 
Huyo ndo anaakili sio haya matakataka ya Tanzania sijui dayamond,masanja mkandamizaji aka tapeli la dini, sijui siwema sepetu aka muuza ngada na mengine yote ya aina hio.
Ni msanii Gani hapa bongo anaweza kuwakatalia vigogo wa nchi hii, msipende kuwaponza wenzenu Ili wawafurahishe huku wakijichimbia kaburi
 
Huku kwetu watakoa kosa hiyo nafasi watakavyowaona wenzao wanaa lOL
 
Nkem Owoh maarufu kama Osuofia alikuwa na rafiki yake marehemu Sam Loco Efe walikuwa wanaigiza vizuri sana.

Huyo Atiku Tinubu ni mzee kutoka chama tawala cha sasa. Kati ya wagombea wa Nigeria ambao siwapendi ni huyu mzee. Chama chao wajinga sana hadi sasa hivi magaidi wanaelekea kushambulia Abuja na vyombo vyote vya ulinzi vipo tu. Uchumi wa Nigeria umefeli, inflation, nauli zimepanda sana, mafuta serikali imelazimika itoe subsidies maana nchi inauza ghafi kwenda nje na inanunua yaliyochakatwa kwa gharama. Imelazimika iyauze kwa hasara kipindi hiki wananchi wasiandamane.

Mgombea mwenyewe kusimama wima hawezi. Huyu ni version mpya ya Buhari, careless hawana muda na raia
20220726_001745.jpg
 
Ingekuwa hapa kwetu huyu msanii angetekwa ama kuuawa. Ndiyo maana hawakataagi
Kama hujui jambo ni vyema ukanyamaza. Hivi unajua Diamond alisaidiwa na JK mwaka 2010 ili kufika alipo? Baada ya Diamond kuhusika kikamilifu katika kampeni za JK.
 
Kama hujui jambo ni vyema ukanyamaza. Hivi unajua Diamond alisaidiwa na JK mwaka 2010 ili kufika alipo? Baada ya Diamond kuhusika kikamilifu katika kampeni za JK.
Sasa umeandika nn hapa? Mm naongelea msanii kukataa kujihusisha na siasa ili kulinda brand. Wewe unaongelea msanii kusaidiwa na mwanasiasa kupata brand. Vinaendana ???
 
Lakini milioni 54 mbona ni hela ndogo sana kwa msanii nguli kama huyu?
Ningeshangaa angekubali.
 
Nkem Owoh maarufu kama Osuofia alikuwa na rafiki yake marehemu Sam Loco Efe walikuwa wanaigiza vizuri sana.

Huyo Atiku Tinubu ni mzee kutoka chama tawala cha sasa. Kati ya wagombea wa Nigeria ambao siwapendi ni huyu mzee. Chama chao wajinga sana hadi sasa hivi magaidi wanaelekea kushambulia Abuja na vyombo vyote vya ulinzi vipo tu. Uchumi wa Nigeria umefeli, inflation, nauli zimepanda sana, mafuta serikali imelazimika itoe subsidies maana nchi inauza ghafi kwenda nje na inanunua yaliyochakatwa kwa gharama. Imelazimika iyauze kwa hasara kipindi hiki wananchi wasiandamane.

Mgombea mwenyewe kusimama wima hawezi. Huyu ni version mpya ya Buhari, careless hawana muda na raiaView attachment 2311697
Lifeless,,,
 
Msanii gani wa Bongo atakataa shilingi za kitanzania milioni 55? Hiyo hela inaweza kuwanunua hata hao wanasiasa wenu mnaowapigia kelele humu. Acheni masihara nyinyi!
 
Back
Top Bottom