Nigeria: Rais Tinubu aanguka wakati akipanda gari la gwaride

Nigeria: Rais Tinubu aanguka wakati akipanda gari la gwaride

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Rais Bola Tinubu wa Nigeria alijikwaa na kuanguka leo 12/6/2024 alipokuwa akipanda gari la gwaride katika Uwanja wa Eagles.

Tinubu alianguka na kujipigiza kichwa wakati wa maadhimisho ya Siku ya Demokrasia ya Juni 12.

Haikuwa wazi kutoka kwenye video ya kuanguka kwake kama kutokana na mavazi yake ya agbada yaliyokuwa yakipepea, na hivyo kusababisha aanguke au alikuwa akipambana na kutembea kwa shida kutokana na uwezekano wa kuwa na afya mbaya.

Walinzi waliokuwa karibu naye hawakuweza kumzuia Rais Tinubu asianguke na kugonga sakafu ya gari.

 
Ndugu zangu Watanzania,

Kuna video nimeiona kwenye ukurasa wa Twitter wa Maulidi Kitenge ikimuonesha Rais wa Nigeria Mheshimiwa Tinubu akianguka chini wakati akitaka kupanda gari. ambapo ni kama alijikwaa na hivyo kumpelekea kwenda chini pasipo kupata msaada wa haraka wa kumdaka kutoka kwa walinzi wake.

Kwa mujibu wa Maulidi Kitenge anadai kuwa wa Nigeria wamewalaumu sana walinzi wake ambao walishindwa kuwa makini ,hasa kwa kutambua kuwa hali ya kiafya ya Rais wao haijawa njema sana tokea kuingia kwake madarakani.

Mimi naishia hapa hapa tu ndugu zangu. Ila nilikuwa naona viongozi wetu wa kiafrika wakiona umri umekwenda sana na hawapo vizuri kiafya ,ni bora kukaa pembeni na kubakia kama washauri tu kwa mamlaka pale inapobidi kama ambavyo alifanya Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere. Japo kujikwaa na kuanguka chini ni bahati mbaya na anaweza kuanguka yeyote yule.

Lakini ukiangalia kwa hali ya kibinadamu unaona wazi kabisa Mheshimiwa Tinubu anahitaji kupata muda mzuri wa kupumzika na kujiangalizia kwa ukaribu afya yake.kuliko kukimbizana na mikiki mikiki ya uongozi na safari za mara kwa mara za kiserikali ambazo inakuwa ni hatari kwa afya yake ,hasa kwa kuzingatia umri wake na hali yake kwa ujumla kiafya.Ok Mungu amsaidie tu na kumtia nguvu.

Video tayari imeshawekwa humu na wadau. Kwenye post Namba 23 .kwa hiyo shuka hapo chini uiangalie vizuri kwa macho yako.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa.Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
 
Naona ni kama amejikwaa hapo na uvaaji wa hilo vazi umechangia sababu mkono wake mmoja wa kulia alikuwa ameshika vazi, na mwingine wa kushoto amejishika na kingo ya hilo gari, so hakuwa na balance na ulizingatia walinzi hawakuwa karibu nae tena walikuwa nyuma.

Lakini uzee nao pia.....
 
Huna kitu kingine cha kuandika zaidi ya propaganda za siasa??
Andika wewe hicho kingine unachotaka wewe. Kwani hili ni jukwaa la nini kwa akili yako? Kama hutaki habari za siasa basi ondoka na nenda haraka sana kwenye majukwaa mengine unayotaka kupata habari zake.
 
Ni kweli uzee na afya pia haipo imara sana.angewaachia wengine washike usukani ili aendelee kujiimarisha kiafya kuliko kukimbizana na mikiki mikiki ya uongozi na safari za hapa na pale za kiserikali.
Kabisa hiyo nafasi si ya kupumzika, umri na majukum haviendani. Nigeria wafanye reforms hii sio nzuri kwa taswira ya nchi
 
Naona ni kama amejikwaa hapo na uvaaji wa hilo vazi umechangia sababu mkono wake mmoja wa kulia alikuwa ameshika vazi, na mwingine wa kushoto amejishika na kingo ya hilo gari, so hakuwa na balance na ulizingatia walinzi hawakuwa karibu nae tena walikuwa nyuma.

Lakini uzee nao pia.....
Madera mwanaume mzima anavaaje nguo na ashikilie
 
Back
Top Bottom