Nigeria: Rais Tinubu aanguka wakati akipanda gari la gwaride

Ifike mahali hawa wazee waachane na madaraka wanatafutia watu lawama tu. Yaleyale ya mwenzie aliyejikojolea waliosambaza video wakauawa.
Na si Tunubu pekee wapo viongozi wengine walowahi kuanguka wakipanda ndege au gari.

1. Marehemu Robert Mugabe- mwaka 2015 alianguka uwanjani Harare.

2. Joe Biden kaanguka mara tatu ndani ya mwaka mmoja wa 2021 akipanda Air Force One.

3. Mwaka 2015 Barak Obama akiwa raisi kijana lakini akakosea ngazi za ndege ya Air Force One na kuanguka. Obama alikuwa ana tabia ya kukimbia kwa madoido akipanda ndege kabla ya kupungia.

4. Marehemu Fidel Castrol alianguka mwaka 2004 akiwa jukwaani.

5. Mwaka 2011 akiwa waziri wa mambo ya nje Hillary Clinton alianguka akipanda ngazi za ndege akiendaYemen na ni msaidizi wake ndiye aliemuokoa kwa kumpa mkono.

6. Yupo mbunge mmoja wa Alabama wa Republican huko Marekani aitwae Tommy Tuberville ambae alimcheka sana raisi Joe Biden kwa kuanguka kila mara, nae akaanguka akipanda ndege mwaka jana.

8. Mike Pence ambae alikuwa makamu wa Donald Trump nae alianguka mwaka 2020 akikimbia kupanda Air Force Two.

9. Miaka ya nyuma kidogo kuna kiongozi mwingine wa Afrika aliwahi kuanguka akiwa jukwaani nimemsahau jina.
 

Mtu umezeeka hata kutembea ni shida na bado unautaka urais.
Hapo kuwalaumu walinzi ni kuwaonea tu, walinzi wote walikuwa chini.
 
Tinubu Kama Biden

Wote wameanguka
 
Biden alidondoka pia

Hata jakaya alidondoka pale jangwani

Ni bahati mbaya
 

Baada ya tukio hilo lililozua taharuki kwa raia mitandaoni, rais alitoa hotuba nzito kuadhimisha Siku ya Demokrasia yaani 12 June kila Mwaka :

wafanyakazi wa mgomo wa kitaifa, hatukutafuta kuwakandamiza au kuwakandamiza wafanyakazi kama serikali ya kidikteta ingefanya. Tulichagua njia ya ushirikiano badala ya migogoro.

45. Hakuna aliyekamatwa au kutishiwa. Badala yake, uongozi wa wafanyikazi ulialikwa kumega mkate na kujadiliana kuelekea azimio la nia njema.

46. Majadiliano ya busara na maelewano ya kanuni ni alama za demokrasia. Mada hizi zitaendelea kuhuisha sera zangu na mwingiliano na sehemu kuu za uchumi wetu wa kisiasa.

47. Ninachukua jukumu hili muhimu bila woga au upendeleo na ninajitolea kwa kazi hii hadi tutakapojenga Nigeria ambapo hakuna mtu anayekandamizwa.

48. Mwishowe, ukuu wetu wa kitaifa hautapatikana kwa kusafiri kwa njia rahisi. Inaweza kupatikana tu kwa kuchukua hatua moja sahihi.

49. Maneno ya Rais wa Marekani Franklin Roosevelt hakika ni ya kweli:

"Kuna njia nyingi za kwenda mbele. Lakini njia moja tu mbaya ni ya kusimama tuli”!

50. Hatuthubutu kusinzia ili mambo mazuri yanayojongea maisha yetu yajayo yasitupite. Hatukubali kuchomeka miguu yetu katika hali ya utulivu kukubali kuishi hapo katikati ya makutano ya matumaini na kukata tamaa.

51. Sisi tunaijua njia iliyo sawa na tutaishika!

52. Miale ya awali ya kesho angavu zaidi ya sasa inaonekana kwenye upeo wa macho mapema. Wakati ujao ni mwingi na uwezo wetu wa kufikia wakati huo ujao upo ndani ya uwezo wetu. Demokrasia na taasisi inazozianzisha zinajitolea kutupeleka kwenye eneo letu la kina muhimu cha demokrasia.

53. Hebu tupande treni hii inayoendelea pamoja. Kwa pamoja, tusonge mbele Nigeria.

54. Tuendelee na moto wa demokrasia. Tuwashe mwenge vizazi na vizazi.

55. Mungu aendelee kubariki Jamhuri ya Shirikisho la Nigeria na kuhifadhi demokrasia yetu.

56. Nawatakia nyote Siku Njema ya Demokrasia.



RAIS BOLA AHMED TINUBU, GCF

 
Hii inaweza mtokea mtu yoyote na hapo mbona ni kama nguo ndio iliyomwangusha ni bahati mbaya tu
 
Aisee, itakuwa kajipigiza vibaya...nadhani anaugulia huyu , inaonekana afya yake ni mgogoro kabisa.
 
Ni kweli uzee na afya pia haipo imara sana.angewaachia wengine washike usukani ili aendelee kujiimarisha kiafya kuliko kukimbizana na mikiki mikiki ya uongozi na safari za hapa na pale za kiserikali.
Wewe mpambe wa Chura achana Bola Tinubu hajaiba Kura.
 
Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa.Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
We jamaa bhana....
 
Ni mdogo Lionel Richie kwa miaka miwili huyo dingi .
 
Mbona Biden na Trump wanagombea. Biden angemuachia Gavin Neewson Governorwa California. Na Trump angemuachia Ron Desantis Governor wa Florida. Lakini bado wanang'angania tu.

Kiranga T14 Armata Nguruvi3
Dunia kwa sasa haina machafuko na ubabe kama zamani. Miaka ya kina Napoleon hakuna superpower angekubali aongozwe na top officials wazee na wana vitambi kama hawa Trump na Biden.
Miaka ile ilikuwa kawaida kiongozi kuwa na miaka 31.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…