Nigeria: Serikali kukopa zaidi ya Dola Bilioni 10 kufadhili Bajeti

Nigeria: Serikali kukopa zaidi ya Dola Bilioni 10 kufadhili Bajeti

kabisa.
buhari kaharibu nchi kuliko watangulizi wake.
serikali inawashughulikia zaidi wanaotaka kujitenga kuliko inavyowashughulikia bandits na fulan.
hivi karibuni umoja wa falme za kiarabu ulianika majina ya watu wanaofadhili ugaidi naijeria but serikali ime mute, haitaki kuwashughulikia.
insecurity iliyopo naijeria inabaraka ya baadhi ya watumishi wakubwa wa serikali.
Ndoto ya Biafra itatimia hata kama si leo

Heri Nchi angeendelea kuishika Goodluck Edibe Jonathan tuu,maana Nchi ilitulia kiuchumi na usalama.

Sent using Jamii Forums mobile app
Huyu Jonathan alikuwa naye wa hovyo tu, kumbuka ghasia za kidini huko Jos, pia ugaidi wa bokoharam ulishamiri kipindi chake (rejea utekaji wa wasichana kule Chibok)

Buhari ana madhaifu yake ila matatizo ya Nigeria hayawezi kupatiwa suluhu ndani ya usiku mmoja.
 
Ugaidi wa bokoharam umepungua?
hakuna USALAMA naijeria.
kuna insurgents wa BH wanajisalimisha kwa serikali lakini ilo ni tone katika bahari.
mbali na Boko haram kuna:-
ISWAP.
HERDMENS.
IPOB.
BANDITS.
HERDMENS hao ni untouchable wanafanya wanavyotaka.
wakati wa Jonathan hawakufikia kiwango iki cha jeuri kama ilivyo sasa.
Nadhani mkuu wa nchi kutoka katika jamii yao na imani yao imechangia wao kufanya lolote wanalojisikia.

BANDITS wao ni wazee wakupora na kuteka watu na kuomba Ransons.
hivi karibuni ndani ya mwezi mmoja afisa mkubwa wa jeshi alitekwa ofisini kwake, watekaji wanaomba pesa na haikupita siku wafanyakazi kadhaa wa Obasanjo wakatekwa.
hao ni kwa uchache tu.
kuna list ndefu ya raia kutekwa etc lakini serikali haijali.
ukipita pita kwenye magroup yao ya whatsapp na jukaa lao(NL) utacheka vile naijeria ilipo kwasasa.
kuna miji baadhi shughuli za kiserekali zinafungwa kwasababu usalama hakuna.

IPOB nao wanafanya uhalifu ili kuhalalisha madai yao ya kujitenga.
Nmandi Kanu alikuwa hakiwahamasisha Ipob ku-boycott shughuli za kiserekali na kuvamia vituo vya police nk.
wameua police sana na wao police imewaua sana.
Nmandi Kanu sasa hivi yupo gwanta. serikali ya buhari ilimuingiza kingi kama vile Mr slim alivyomuingiza kingi yule jamaa aliyegeuziwa ndege angani, suddenly anashangaa pipa imetua Kigali.
dual citizenship ya Uk na Naijeria ilimpa kiburi, kahuska indirectly katika mamia ya mauaji. sijui nini kilimtoa Uk hadi kenya, serikali ya kenyata ikafanya yake, akadakwa.
itoshe kusema Somalia ina unafuu kuliko naijeria kwa upande wa Usalama.

Screenshot_20211009-182014_Nairaland Forum.jpg
 
itoshe kusema Somalia ina unafuu kuliko naijeria kwa upande wa Usalama.
Duh!...Somalia hii hii ya Alshabaab

Anyway nadhani hali hiyo ya kudorora kwa usalama inachangiwa kwa kiasi kikubwa na siasa za ndani ya nchi, mfano kuna kipindi ilisemekana baadhi ya wanasiasa hupuuza baadhi ya taarifa za kiusalama kwa kudhani kuchukua hatua kutawanufaisha mahasimu wao.

Hata serikali ya Jonathan inasemekana ilizembea kuchuka hatua dhidi ya bokoharam kwa kudhani ilikuwa ni siasa za watu wa kaskazini kuidhoofisha serikali yake, mpaka ilipoamua kukodisha askari mamluki kutoka Africa kusini na ulaya mashariki kuongeza shinikizo kwa bokoharam ilipokaribia kipindi cha uchaguzi japo Jonathan alishindwa uchaguzi.

Kuna kipindi serikali ya Buhari ilijipata imefanikiwa kuwadhoofisha bokoharam ila cha ajabu matukio ya utekaji yaliibuka mengi sana.

Nigeria ni nchi tu, ila huwezi kusema ni taifa maana ina mgawanyiko mkubwa mno.
 
"Nigeria ni nchi tu, ila huwezi kusema ni taifa maana ina mgawanyiko mkubwa mno".

huu ndiyo uhalisia.
 
Rais Muhammadu Buhari amesema Serikali imepanga kukopa zaidi ya Dola za Marekani Bilioni 10 ili kusaidia kufadhili Bajeti ya takriban Dola Bilioni 40 kwa mwaka 2022

Kumekuwa na malalamiko kuhusu Mikopo ya mara kwa mara ya Serikali lakini Rais Buhari ameendelea kusisitiza kiwango bado ni himilivu

Nigeria kwa kiasi kikubwa inategemea usafirishaji wa mafuta ghafi kwa mapato yake

======

Nigeria’s President Muhammadu Buhari says the government plans to borrow more than $10bn (£7.3bn) to help finance his 2022 budget of nearly $40bn.

There has been a public outcry about the government's frequent borrowing, but Mr Buhari - in a presentation to parliament - said that Nigeria’s debt level was still within sustainable limits.

Presenting the budget is an annual ritual, but there aren't enough reports about how the money is spent.

Nigeria’s economy is plagued by high inflation as the local currency continues to lose value against major foreign currencies like the US dollar and pound sterling.

Nigeria is mainly dependent on the export of crude oil for its revenue.

Source: BBC
Uchumi ulifika negative growth hawana ujanja lazima wakope..Tzn tutakoba dola bil.1.1 sawa na asilimia 1.5 ya GDP kwa ajili ya kuimarisha reserves ya fedha za kigeni.
 
Uchumi ulifika negative growth hawana ujanja lazima wakope..Tzn tutakoba dola bil.1.1 sawa na asilimia 1.5 ya GDP kwa ajili ya kuimarisha reserves ya fedha za kigeni.
Ina maana kulikuwa hakuna ukuaji wowote zaidi ya mdororo tu?...au Covid-19 ilishusha sana bei ya mafuta?
 
Back
Top Bottom