Nigeria: Serikali kukopa zaidi ya Dola Bilioni 10 kufadhili Bajeti


Heri Nchi angeendelea kuishika Goodluck Edibe Jonathan tuu,maana Nchi ilitulia kiuchumi na usalama.

Sent using Jamii Forums mobile app
Huyu Jonathan alikuwa naye wa hovyo tu, kumbuka ghasia za kidini huko Jos, pia ugaidi wa bokoharam ulishamiri kipindi chake (rejea utekaji wa wasichana kule Chibok)

Buhari ana madhaifu yake ila matatizo ya Nigeria hayawezi kupatiwa suluhu ndani ya usiku mmoja.
 
Ugaidi wa bokoharam umepungua?
hakuna USALAMA naijeria.
kuna insurgents wa BH wanajisalimisha kwa serikali lakini ilo ni tone katika bahari.
mbali na Boko haram kuna:-
ISWAP.
HERDMENS.
IPOB.
BANDITS.
HERDMENS hao ni untouchable wanafanya wanavyotaka.
wakati wa Jonathan hawakufikia kiwango iki cha jeuri kama ilivyo sasa.
Nadhani mkuu wa nchi kutoka katika jamii yao na imani yao imechangia wao kufanya lolote wanalojisikia.

BANDITS wao ni wazee wakupora na kuteka watu na kuomba Ransons.
hivi karibuni ndani ya mwezi mmoja afisa mkubwa wa jeshi alitekwa ofisini kwake, watekaji wanaomba pesa na haikupita siku wafanyakazi kadhaa wa Obasanjo wakatekwa.
hao ni kwa uchache tu.
kuna list ndefu ya raia kutekwa etc lakini serikali haijali.
ukipita pita kwenye magroup yao ya whatsapp na jukaa lao(NL) utacheka vile naijeria ilipo kwasasa.
kuna miji baadhi shughuli za kiserekali zinafungwa kwasababu usalama hakuna.

IPOB nao wanafanya uhalifu ili kuhalalisha madai yao ya kujitenga.
Nmandi Kanu alikuwa hakiwahamasisha Ipob ku-boycott shughuli za kiserekali na kuvamia vituo vya police nk.
wameua police sana na wao police imewaua sana.
Nmandi Kanu sasa hivi yupo gwanta. serikali ya buhari ilimuingiza kingi kama vile Mr slim alivyomuingiza kingi yule jamaa aliyegeuziwa ndege angani, suddenly anashangaa pipa imetua Kigali.
dual citizenship ya Uk na Naijeria ilimpa kiburi, kahuska indirectly katika mamia ya mauaji. sijui nini kilimtoa Uk hadi kenya, serikali ya kenyata ikafanya yake, akadakwa.
itoshe kusema Somalia ina unafuu kuliko naijeria kwa upande wa Usalama.

 
itoshe kusema Somalia ina unafuu kuliko naijeria kwa upande wa Usalama.
Duh!...Somalia hii hii ya Alshabaab

Anyway nadhani hali hiyo ya kudorora kwa usalama inachangiwa kwa kiasi kikubwa na siasa za ndani ya nchi, mfano kuna kipindi ilisemekana baadhi ya wanasiasa hupuuza baadhi ya taarifa za kiusalama kwa kudhani kuchukua hatua kutawanufaisha mahasimu wao.

Hata serikali ya Jonathan inasemekana ilizembea kuchuka hatua dhidi ya bokoharam kwa kudhani ilikuwa ni siasa za watu wa kaskazini kuidhoofisha serikali yake, mpaka ilipoamua kukodisha askari mamluki kutoka Africa kusini na ulaya mashariki kuongeza shinikizo kwa bokoharam ilipokaribia kipindi cha uchaguzi japo Jonathan alishindwa uchaguzi.

Kuna kipindi serikali ya Buhari ilijipata imefanikiwa kuwadhoofisha bokoharam ila cha ajabu matukio ya utekaji yaliibuka mengi sana.

Nigeria ni nchi tu, ila huwezi kusema ni taifa maana ina mgawanyiko mkubwa mno.
 
"Nigeria ni nchi tu, ila huwezi kusema ni taifa maana ina mgawanyiko mkubwa mno".

huu ndiyo uhalisia.
 
Uchumi ulifika negative growth hawana ujanja lazima wakope..Tzn tutakoba dola bil.1.1 sawa na asilimia 1.5 ya GDP kwa ajili ya kuimarisha reserves ya fedha za kigeni.
 
Uchumi ulifika negative growth hawana ujanja lazima wakope..Tzn tutakoba dola bil.1.1 sawa na asilimia 1.5 ya GDP kwa ajili ya kuimarisha reserves ya fedha za kigeni.
Ina maana kulikuwa hakuna ukuaji wowote zaidi ya mdororo tu?...au Covid-19 ilishusha sana bei ya mafuta?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…