Nigeria: Taharuki yatanda mitandaoni kutokana na mauaji ya mwanafunzi aliyekuwa akijisomea Kanisani

Nigeria: Taharuki yatanda mitandaoni kutokana na mauaji ya mwanafunzi aliyekuwa akijisomea Kanisani

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
- Mwanafunzi huyo alikuwa anajisomea ndani ya kanisa la Redeemed Christian Church of God (RCCG) wakati wa tukio hilo

- Familia yake ilipokea simu kutoka mama mmoja wa kanisa hilo
- Uwavera alikimbizwa hospitalini baada ya mlinzi kumpata sketi yake ikiwa imechanika na blauzi yake ikiwa imelowa damu

- Alikata roho hospitalini siku ya Jumamosi, Mei 30, kutokana na majeraha aliyopata


Wanigeria wamezua hamaki mitandaoni kufuatia mauaji ya kinyama ya mwanafunzi mwenye miaka 22, Uwavera Omozuwa aliyeuawa kanisani.

Kampeni ya kutaka atendewe haki imeenea kwenye mitandao ya kijamii nchini Nigeria, huku familia yake ikiomba msaada wa kumtafuta muuaji.

Mwanafunzi
Uwavera alikuwa anajisomea ndani ya kanisa la Redeemed Christian Church of God(RCCG) wakati wa tukio hilo. Picha: Yabaleft.

Kulingana na dada yake marehemu,Judith Omozuwa, Uwavera alikuwa anajisomea vitabu vyake ndani ya kanisa la Redeemed Christian Church of God(RCCG), karibu na nyumbani kwao Benin City wakati wa tukio hilo.
Familia yake ilipokea simu kutoka mama mmoja wa kanisa hilo mnamo Jumatano, Mei 27.

Judith alifichua kwamba dada yake mpendwa alibakwa kabla ya kuawa na wahalifu hao.

Mwanafunzi
Uwavera alikua amejiunga na Chuo Kikuu cha Benin kusomea microbiolojia.Picha:Yabaleft.
Dada huyo alisimulia kwamba Uwavera alikimbizwa hospitalini baada ya mlinzi kumpata sketi yake ikiwa imechanika na blauzi yake ikiwa imelowa damu.

Mwanafunzi huyo ambaye alikuwa na ndoto ya kuwa muuguzi, alikata roho hospitalini siku ya Jumamosi, Mei 30, kutokana na majeraha aliyopata baada ya kushambuliwa.

Mwanafunzi
Mwanzilishi wa kanisa la RCCG E.A.Adeboye ameshtumu tukio hilo. Picha: UGC.
Uwavera alikua amejiunga na Chuo Kikuu cha Benin kusomea microbiolojia kabla ya kukumbana na mauti yake.

Dada yake alifichua kwamba marehemu alikuwa na mazoea ya kwenda kujisomea katika kanisa hilo ambalo liko karibu na nyumbani kwao kwa sababu ya utulivu.

Mwanzilishi wa kanisa hilo Pasta E.A. Adeboye alizungumzia kisa hicho cha kinyama na kumtaka kila mmoja kuombea familia ya marehemu ili wapate haki.
 
Inasikitisha sana..binadamu tumekoswa utu hakika.
 
Huwa najiuliza lakini sipati majibu,hivi kama lengo lilikuwa ni kubaka kwanini wakimaliza wamuue?au kama lengo ni kumuua kwanini wambake ndio wamuue,au huwa inatokea wanamuua kwa bahati mbaya akiwa katika harakati za kujitetea...?
 
Back
Top Bottom