SI KWELI Nigeria watu wasio na mahusiano (Single) watafungwa jela

SI KWELI Nigeria watu wasio na mahusiano (Single) watafungwa jela

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Nigeria Single ladies and men wanafungwa kwa kulala siku nzima nakupoteza oxygen ya buree.
Screenshot 2025-07-04 091932.png



 
Tunachokijua
Katika muktadha wa kisheria, mtu ambaye ni 'single' hufafanuliwa kama mtu ambaye hajaoa au kuolewa, hayuko katika uhusiano wa ndoa, na hayuko katika uhusiano wa kimapenzi wa kudumu

Madai

Kumekuwa na kipande cha video kinachosambazwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii ikieleza kuwa serikali ya Nigeria imeanza kuwakamata watu wasio na mahusiano (Single) ya kimapenzi. Miongoni mwa maneno yanayosikika ni;

“Yes have decided to start arresting people who have been single for too long and loneliness is now affecting national productivity” ikiwa na maana kuwa

“Kwa sasa tumeamua kuanza kuwakamata watu wasiokuwa na mahusiano kwa muda mrefu kwani upweke wao unaathiri shughuli za uzalishaji kwenye Taifa’’

Uhalia wa taarifa hiyo

JamiiCheck imefuatilia taarifa hiyo na kujiridhsha kuwa si ya kweli.

Ufuatiliaji umebaini kuwa hakuna chanzo chochote za kuaminika kutoka nchini Nigeria kilichochapisha ama kutoa taarifa hiyo.

Aidha vipande hivyo vya video vimetengenezwa kwa teknolojia ya Akili Unde (AI). Sauti zinazosikika katika video hizo ni za kutengenezwa pia kwa akili unde. Unaweza kurejelea baadhi ya maneno yanayoonekana kwenye video hizo hayana mpangilio mzuri hivyo kupoteza maana.

Ufuatilaji kwa kutumia nyenzo za kidijitali umebainisha kuwa sauti inayosikika imetengenzwa kwa kutumia akili unde kwa zaidiya 90%.
Why staying single!!?
Kule kwa King Mswati, mwanaume lazima kuoa demu tano.
 
Back
Top Bottom