Nigeria yaacha kununa, ipo tayari kujiunga na Waafrika wengine, pia Kiswahili chateuliwa kama lugha rasmi ya Afrika

Haya basi, tumia kingereza kuzungumza nasi kwa kuwa Kiswahili kimetushinda.

Ukizungumza au kuwasiliana na beans zenu Mzansi/Afrika Kusini mnakitumia Kiswahili?
 
Mi niwashauri tu msije mkawafundisha wenzenu kuwa Nyanya ni Grandmother, tafadhalini NYANYA ni tomato ile vegetable. Bibi ni grandmother, na ukitaka kumwambia mtu Sit Down sio Keti chini, ni "kaa chini" ndio kiswahili original
Lol.. Kwani kiswahili cha Tanzania hakiruhusu synonyms? Duh!
Hebu mmoja wenu atuwekee mtihani wa kiswahili wa kidato cha NNE TZ. Nitaleta wa KE. tulinganishe.
GODZILLA
 
Lol.. Kwani kiswahili cha Tanzania hakiruhusu synonyms? Duh!
Hebu mmoja wenu atuwekee mtihani wa kiswahili wa kidato cha NNE TZ. Nitaleta wa KE. tulinganishe.
GODZILLA
Hizo ni lahaja tu. 'Keti' au 'Kaa' ni kitu kile kile lakini ni watanzania wachache wanatumia hiyo 'keti'.

Ndio maana nikamwambia yule ndugu yako MK254 ana Kiswahili cha 'kiroboti' kwa sababu ya matumizi ya maneno kama 'keti' na mengine yenye mfanano huo.

Kuna maneno ukitumia unaonekana una 'mechanical language'. Hauna lugha 'laini'. Ni kama roboti aliyechakatwa.
 
Kiswahili kina kupa shida... Kaka pambana na hii lugha kwanza...
 
Naomba uniletee mtihani wowote wa kiswahili .I want to see the difference
 

Hao Zambia, Zimbabwe n.k. hayo majina na mipaka yao yote kazi ya mkoloni, mababu zetu Afrika waliishi ndani ya makabila yao, hamna jinsi unaweza kuniamisha kuna undugu wowote baina Mnyamwezi na Mzaramo, ni kwamba mzungu alibuni taifa kwa kuchora mipaka kisha akawakusanya makabila na kuwapa utaifa.
Siku mtakombolewa huo utumwa mamboleo, ndio mtaelewa nini kinafanyika.
 
Zimbabwe = South Rhodesia
Zambia= North Rhodesia

Pure African names
 
Nyuma ya huo mkataba yupo xi au Trump.
 
Yote ilikuwa inaitwa Rhodesia,

Zambia ni jina la hiyo nchi hata kabla ya miungu yenu Wakenya kurusha miguu yao Africa na lilitokana na mto Zambezi mkubwa

Zimbabwe ni geographical name maarufu vilevile kama Zambia na ilikuwa ni mji mkubwa sana wa washona waliouita the great Zimbabwe kabla ya Cecil Rhodes kuingia.

Unazidi kunipa uhakika kwamba umevurugwa pakubwa na miungu yako.
 
Mzungu aliamuru tuitwe tanzania? Unawashwa wewe nishakwambiaga. Tanzania is our own designed name, urudi darasani.
 
Nyuma ya huo mkataba yupo xi au Trump.
Ndoto ya mkataba kama huu ndio ilifanya Col. Muamar Ghadaffi atangulizwe mbele ya haki. Hakuna nchi yeyote ya magharibi ambayo ina hamu na mkataba kama huu wa kibiashara kati ya nchi za Afrika. AfCFTA ni mkataba wa soko huru kati ya nchi zote za Afrika, kasoro Tz na Benin, kwa bidhaa zao zinazotoka hapa hapa Afrika.
 
Mjinga sana huyu jamaa
 
Handsets tutanunua toka wapi mkuu!!
 
Hawa jamaa wanapenda sana kutembelea nyota yetu
Tanzanite walijifanya yao,mlima Kilimanjaro wanajifanya upo kwao na sasa wanataka kukifanya kiswahili kiwe chao
kuna siku watasema na tanzania ipo kenya...mimi nawaangalia tuu
 
Handsets tutanunua toka wapi mkuu!!
Jombaa, huu mkataba hautapiga marufuku bidhaa kutoka nje ya bara hili. Ila nchi za afrika zitakuwa zinanua bidhaa ambazo zinalishwa hapa hapa Afrika kwanza kabla ya kujazilia pengo lililosalia na bidhaa kutoka nje ya bara hili.
 
Jombaa, huu mkataba hautapiga marufuku bidhaa kutoka nje ya bara hili. Ila nchi za afrika zitakuwa zinanua bidhaa ambazo zinalishwa hapa hapa Afrika kwanza kabla ya kujazilia pengo lililosalia na bidhaa kutoka nje ya bara hili.
Sipingi maono haya, napenda kujua nani wanatengeneza handsets ili tuanze kujipanga kuachana na vichomi (xiomi)
 
Sipingi maono haya, napenda kujua nani wanatengeneza handsets ili tuanze kujipanga kuachana na vichomi (xiomi)
Xiomi zako bado tutaangiza jombaa, kwasababu kwa sasa havitengenezwi kwenye bara hili. Bidhaa zingine kutoka Afrika zitapewa kipau mbele kabla ya kuagiza kutoka nje. Kwa nchi ambazo zipo kwenye mkataba huu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…