Nigeria yaacha kununa, ipo tayari kujiunga na Waafrika wengine, pia Kiswahili chateuliwa kama lugha rasmi ya Afrika

Nigeria yaacha kununa, ipo tayari kujiunga na Waafrika wengine, pia Kiswahili chateuliwa kama lugha rasmi ya Afrika

Tangu lini manyang'au mkajua Kiswahili? Au zile lugha zenu uchwara za kuokoteza okoteza majalalani ndizo mnaziita Kiswahili? Hebu wacha vihoja.

Manyang'au hamfui dafu Kwenye Kiswahili, kwahiyo msikaze shingo.... badala yake mje Tanzania tuwape twisheni ya sarufi kabla hamjarukia habari za Afrika kusini. Mtatutia aibu.
Haya basi, tumia kingereza kuzungumza nasi kwa kuwa Kiswahili kimetushinda.

Ukizungumza au kuwasiliana na beans zenu Mzansi/Afrika Kusini mnakitumia Kiswahili?
 
Mi niwashauri tu msije mkawafundisha wenzenu kuwa Nyanya ni Grandmother, tafadhalini NYANYA ni tomato ile vegetable. Bibi ni grandmother, na ukitaka kumwambia mtu Sit Down sio Keti chini, ni "kaa chini" ndio kiswahili original
Lol.. Kwani kiswahili cha Tanzania hakiruhusu synonyms? Duh!
Hebu mmoja wenu atuwekee mtihani wa kiswahili wa kidato cha NNE TZ. Nitaleta wa KE. tulinganishe.
GODZILLA
 
Lol.. Kwani kiswahili cha Tanzania hakiruhusu synonyms? Duh!
Hebu mmoja wenu atuwekee mtihani wa kiswahili wa kidato cha NNE TZ. Nitaleta wa KE. tulinganishe.
GODZILLA
Hizo ni lahaja tu. 'Keti' au 'Kaa' ni kitu kile kile lakini ni watanzania wachache wanatumia hiyo 'keti'.

Ndio maana nikamwambia yule ndugu yako MK254 ana Kiswahili cha 'kiroboti' kwa sababu ya matumizi ya maneno kama 'keti' na mengine yenye mfanano huo.

Kuna maneno ukitumia unaonekana una 'mechanical language'. Hauna lugha 'laini'. Ni kama roboti aliyechakatwa.
 
Jaguar anataka sio Wakenya wanataka...mbiba lugha unayojivunia inakuwa ngumu kwako kuielewa?
Nyie ndio wabaguzi wakubwa, angalia vile umeingia kwenye uzi huu kwa hasira. Ni Mwafrika mgani amepigwa au kubaguliwa Kenya ukilinganisha na Wakenya wanaobaguliwa Tanzania? Wacha unafiki na umbea.
Nchi yenu ndiye mbaguzi mkubwa haijangia kwenye huu mkataba wa kuwaunganisha Waafrika wote.
Kiswahili kina kupa shida... Kaka pambana na hii lugha kwanza...
 
Hizo ni lahaja tu. 'Keti' au 'Kaa' ni kitu kile kile lakini ni watanzania wachache wanatumia hiyo 'keti'.
Ndio maana nikamwambia yule ndugu yako MK254 ana Kiswahili cha 'kiroboti' kwa sababu ya matumizi ya maneno kama 'keti' na mengine yenye mfanano huo.
Kuna maneno ukitumia unaonekana una 'mechanical language'. Hauna lugha 'laini'. Ni kama roboti aliyechakatwa.
Naomba uniletee mtihani wowote wa kiswahili .I want to see the difference
 
Nani kasema hivyo? Kulikuwa na Africa trade caravans nyingi tu kati ya makabila yaliyopo kwe present day Tanzania na makabila ya huko Zimbabwe, Zambia ndio maana ukisikiliza kishona cha Zimbabwe ni almost kiswahili kitupu na kuna uthibitisho mkubwa tu wa mambo haya

Unafikiri wakati biashara hiyo ya masafa marefu ikifanyika kutoa chumvi Kigoma kupeleka Harare walikuwa wanatambulika kama wafanyabiashara kutoka wapi?

Tatizo la Waafrika wengi tumemezeshwa upumbavu wa fake history ya mzungu na muarabu hakuna chochote cha maana wanachomuongelea kwacho muafrika zaidi ya udunishaji, upumbavu ambao hata wewe umekupata.

Kuna muarabu fulani alitaka kuiba legacy ya Mtanzania kwamba yeye ndio aliegundua Tanzanite mpaka Wikipedia na mitandaoni kajiandikia history uchwara wakati kitu kiko wazi kabisa ni nani mvumbuzi wa Tanzanite kwa hiyo sishangai eurocentric mediocrity mliyonayo kichwani mwenu, ni janga la dunia.

Poleni

Hao Zambia, Zimbabwe n.k. hayo majina na mipaka yao yote kazi ya mkoloni, mababu zetu Afrika waliishi ndani ya makabila yao, hamna jinsi unaweza kuniamisha kuna undugu wowote baina Mnyamwezi na Mzaramo, ni kwamba mzungu alibuni taifa kwa kuchora mipaka kisha akawakusanya makabila na kuwapa utaifa.
Siku mtakombolewa huo utumwa mamboleo, ndio mtaelewa nini kinafanyika.
 
Zimbabwe = South Rhodesia
Zambia= North Rhodesia

Pure African names
 
Waafrika wote walipokuwa wakiungana nyinyi hapo mlijivimbisha vichwa na hamkutaka kabisa kujihusisha na wenzenu. Sasa lugha ya kiswahili ndio itakuwa lugha rasmi ya biashara Afrika chini ya huu mkataba wa AfCFTA. Nchi ya Kenya pekee ndio imesalia kama nchi inayowakilisha kiswahili kwenye huu muungano wa kibiashara wa nchi za kiafrika. Fursa ndio hizi zinatuandama, mtanuna hadi mfe.
Nyuma ya huo mkataba yupo xi au Trump.
 
Hao Zambia, Zimbabwe n.k. hayo majina na mipaka yao yote kazi ya mkoloni, mababu zetu Afrika waliishi ndani ya makabila yao, hamna jinsi unaweza kuniamisha kuna undugu wowote baina Mnyamwezi na Mzaramo, ni kwamba mzungu alibuni taifa kwa kuchora mipaka kisha akawakusanya makabila na kuwapa utaifa.
Siku mtakombolewa huo utumwa mamboleo, ndio mtaelewa nini kinafanyika.
Yote ilikuwa inaitwa Rhodesia,

Zambia ni jina la hiyo nchi hata kabla ya miungu yenu Wakenya kurusha miguu yao Africa na lilitokana na mto Zambezi mkubwa

Zimbabwe ni geographical name maarufu vilevile kama Zambia na ilikuwa ni mji mkubwa sana wa washona waliouita the great Zimbabwe kabla ya Cecil Rhodes kuingia.

Unazidi kunipa uhakika kwamba umevurugwa pakubwa na miungu yako.
 
Kila taifa ndani ya Afrika yote ni shithole, tumetukanwa vya kutosha, ndio maana tumeamua kufanya kitu kinachoitwa reset, tuanze upya, muamko mpya, soko la watu zaidi ya bilioni moja kutegemeana bila mipaka tuliyochorewa na mzungu kisha akageuza.
Wewe hapo Mzungu aliamuru muitwe Watanzania, huku akasema tuitwe Wakenya, baadhi ya makabila yetu mpakani hapo, watu wa kabila moja, ndugu kabisa lakini wanaonana kwa misingi ya mipaka waliyowekewa, hauwezi kumuuzia chochote mjomba wako ndugu wa damu wa baba yako kisa yupo upande wa pili wa mpaka wa kikoloni.
Hivyo muungano huu sio ligi mlizozoea, hatupo kushindana na Nigeria wala taifa lolote, tunaungana ili tuandike historia upya.
Mzungu aliamuru tuitwe tanzania? Unawashwa wewe nishakwambiaga. Tanzania is our own designed name, urudi darasani.
 
Nyuma ya huo mkataba yupo xi au Trump.
Ndoto ya mkataba kama huu ndio ilifanya Col. Muamar Ghadaffi atangulizwe mbele ya haki. Hakuna nchi yeyote ya magharibi ambayo ina hamu na mkataba kama huu wa kibiashara kati ya nchi za Afrika. AfCFTA ni mkataba wa soko huru kati ya nchi zote za Afrika, kasoro Tz na Benin, kwa bidhaa zao zinazotoka hapa hapa Afrika.
 
Hahaha usitake nicheke

Jina Tanganyika lina history yake ndefu tu kama jina Kilimanjaro na majina mengi maarufu Tanzania

Kwa Taarifa yako jina Tanganyika wala sio legacy ya mzungu, limetokana na maneno ya kibantu TANGA - sehemu yenye maji na upepo mwingi au bahari na neno NYIKA - sehemu kubwa ya nchi kavu isio na vyanzo vya maji,

Usikurupuke kwa kuongea usiyoyajua naona ungedeal na mambo ya nchi yako kuliko kujidai unaijua sana Tanzania wakati huna ulijualo.
Mjinga sana huyu jamaa
 
Ndoto ya mkataba kama huu ndio ilifanya Col. Muamar Ghadaffi atangulizwe mbele ya haki. Hakuna nchi yeyote ya magharibi ambayo ina hamu na mkataba kama huu wa kibiashara kati ya nchi za Afrika. AfCFTA ni mkataba wa soko huru kati ya nchi zote za Afrika, kasoro Ty na Benin, kwa bidhaa zao zinazotoka hapa hapa Afrika.
Handsets tutanunua toka wapi mkuu!!
 
Hawa jamaa wanapenda sana kutembelea nyota yetu
Tanzanite walijifanya yao,mlima Kilimanjaro wanajifanya upo kwao na sasa wanataka kukifanya kiswahili kiwe chao
kuna siku watasema na tanzania ipo kenya...mimi nawaangalia tuu
 
Handsets tutanunua toka wapi mkuu!!
Jombaa, huu mkataba hautapiga marufuku bidhaa kutoka nje ya bara hili. Ila nchi za afrika zitakuwa zinanua bidhaa ambazo zinalishwa hapa hapa Afrika kwanza kabla ya kujazilia pengo lililosalia na bidhaa kutoka nje ya bara hili.
 
Sipingi maono haya, napenda kujua nani wanatengeneza handsets ili tuanze kujipanga kuachana na vichomi (xiomi)
 
Sipingi maono haya, napenda kujua nani wanatengeneza handsets ili tuanze kujipanga kuachana na vichomi (xiomi)
Xiomi zako bado tutaangiza jombaa, kwasababu kwa sasa havitengenezwi kwenye bara hili. Bidhaa zingine kutoka Afrika zitapewa kipau mbele kabla ya kuagiza kutoka nje. Kwa nchi ambazo zipo kwenye mkataba huu.
 
Back
Top Bottom