Nigeria yapiga marufuku wanamitindo na sauti za kigeni

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Habari na Utamaduni ya Shirikisho nchini humo imesema serikali inataka kulinda vipaji vya ndani na kukuza uchumi.

Kwa mujibu wa Wizara ya Habari, kuanzia sasa watangazaji, matangazo na bidhaa zote za masoko na mawasiliano nchini humo zinatakiwa kuwatumia waandaaji na wasanii wa ndani pekee.

Utekelezaji wa agizo hilo ambalo halitahusu kampeni na matangazo yanayoendelea kwenye vyombo vya Utangazaji, utaanza rasmi Oktoba 1, 2022.

==============================
1661279054876.png
 
Ilhali hapa Tanzania Serikali inapambana kuhakikisha wageni wanachota Rasilimali zetu wanavyojisikia.
 
Kwa nini serikali inaingilia biashara za watu? Kama Dangote anataka kumtumia Obama kwenye matangazo ya biashara zake, kwa nini akatazwe?
 
Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Habari na Utamaduni ya Shirikisho nchini humo imesema serikali inataka kulinda vipaji vya ndani na kukuza uchumi.

Kwa mujibu wa Wizara ya Habari, kuanzia sasa watangazaji, matangazo na bidhaa zote za masoko na mawasiliano nchini humo zinatakiwa kuwatumia waandaaji na wasanii wa ndani pekee.

Utekelezaji wa agizo hilo ambalo halitahusu kampeni na matangazo yanayoendelea kwenye vyombo vya Utangazaji, utaanza rasmi Oktoba 1, 2022.

==============================
View attachment 2332857
Upuuzi. Sasa na mataifa ambayo wasanii wa Nigeria wanapiga pesa ndefu nao wakisema ni matufuku kwa Wanaigeria kufanya kazi za sanaa zikiwemo za kimuziki na matangazo ya baishara itakuwaje?ni nani atakuwa ameumia?
 
Back
Top Bottom