Nigeria yapiga marufuku wasafiri kutoka India, Brazil na Uturuki

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Kamati ya rais ya kupambana na janga la Covid-19 nchini Nigeria, imesema taifa hilo litapiga marufuku wasafiri wanaokuja kutoka India, Brazil na Uturuki, kutokana na kuenea pakubwa kwa virusi vya corona katika mataifa hayo.

Taarifa ya mwenyekiti wa kamati hiyo Boss Mustapha, imesema watu walio na hati za kusafiria zisizo za Nigeria na wasiokuwa wakaazi wa taifa hilo waliozuru mataifa yaliotajwa katika kipindi cha siku 14 kabla ya kwenda Nigeria, watanyika ruhusa ya kuingia nchini humo, kuanzia Mei 4.

Nigeria imetangaza visa vipya 43 vya maambukizi ya virusi vya corona jana Jumamosi, na kufanya jumla ya visa vyake kuwa 165,153, na vifo 2,063.

DW
 
Bora wangepiga marufuku wabrazili na wahindi. Lakini sio uturuki.
 
Tishio hapa kwetu na wanao safiri kutoka Uturuki na India - wataalamu wa ujenzi wa SGR wanatoka Uturuki na ndege ya Uturuki sijui inaingia mara ngapi hapa kwa wiki, wapo vile vile wafanya biashara wakazi wa Kituruki wengi tu hapa Dar - kinacho tisha zaidi siku za karibuni visa vya kukamatwa kwa meli/mashua zilizo sheheni madawa ya kulevya huku zikizinguka zunguka katika mwambao wa pwani ya Tanzania zimeongezeka sana, meli hizo zinatoka India na Pakistan penye ugonjwa huu wa variant mpya ya covid - je, hao wa Pakistan na wahindi wapo usalama gani Kiafya dhidi ya Covid - tuwe makini kudhibiti kweli kweli uingiaji nchini kwa jamaa hawa wasije wakatuletea balaaa.
 
Ila huku sisi tuna undugu na covid-19 naona wala hakuna zuiyo
 


Miss zomboko, changia hata kanukta basi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…