carbohydates
JF-Expert Member
- Oct 13, 2026
- 260
- 607
Nigeria imethibitisha uwepo wa mgonjwa wa kwanza cha Ebola katika mlipuko wa sasa baada ya mwanamke aliyesafiri kutoka Uganda kupatikana na maambukizi ya ugonjwa huo.
Waziri wa Afya wa Nigeria, Muhammad Ali Pate, amesema vipimo vya maabara vimethibitisha maambukizi hayo na mgonjwa amewekwa karantini kwa ajili ya matibabu na uangalizi.Mamlaka za afya nchini humo zimebaini watu 44 waliokuwa na mawasiliano ya karibu na mgonjwa huyo na zimeanza kuwafuatilia ili kudhibiti uwezekano wa kuenea kwa maambukizi.
Nigeria ni nchi ya kwanza ya Afrika Magharibi kuripoti kisa cha Ebola kinachohusishwa na mlipuko wa sasa unaoendelea katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na maeneo ya Afrika Mashariki. Nchi hiyo ilifanikiwa kudhibiti mlipuko wa ugonjwa huo mwaka 2014, uliosababisha vifo vya watu wasiopungua wanane.
Kwa mujibu wa Kituo cha Ulaya cha Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa (ECDC), mlipuko wa sasa nchini DRC ulioanza Mei umesababisha vifo vya watu wasiopungua 4,600, huku zaidi ya visa 9,500 vikirekodiwa.
Mlipuko huo umesababishwa na aina ya virusi vya Ebola vinavyojulikana kama Bundibugyo, ambavyo ni nadra na havina chanjo wala tiba iliyoidhinishwa kwa sasa, ingawa majaribio ya matibabu yanaendelea.
Ugonjwa huo pia uliripotiwa Uganda, ambako watu wasiopungua wawili walifariki, na Kenya, ambayo imeripoti uwepo wa wagonjwa kadhaa.
Ebola huambukizwa kupitia majimaji ya mwili wa mtu aliyeambukizwa, yakiwamo damu na matapishi. Dalili zake ni pamoja na kutapika na kuharisha, na katika hali kali inaweza kusababisha kushindwa kufanya kazi kwa viungo vya mwili na kutokwa na damu.
Chanzo: Tbc Digital