Nigeria yatolewa! Stars washindwe wenyewe tu!

acha kuota ndoto za mchana.....
 
sasa hv kundi la stars inaenda timu moja badala ya 2 nafasi bado ngumu hila nigeria sababu washapoteza wasitukomalie sana.
Nigeria haijashinda mechi hata moja yani akubali kuondoka na vipointi viwili tuu? Naona watakomaa sana kuondoka na ushindi kwakuwa wanacheza kwao. Draw ya hapa ndo inatuweka katika wakati mgumu tena tupo ugenini na bahati mbaya sisi hatuna utamaduni wa kusafiri na timu yetu kuishangilia ikiwa ugenini kwasababu mbalimbali kama uchumi mdogo nk...

Mchezo wa soka nchini hauna mafanikio hususani kwa timu ya taifa. Hili ni tatizo linalosababishwa na mambo mengi kwanza naona siasa nyingi kwenye soka letu, morale ndogo ya wachezaji, VPL inamatatizo mengi na migogoro.
Ndiyo maana Taifa stars haina mafanikio yoyote kwa kuwa imeshiriki michuano ya kufuzu kucheza mashindano mengi ila imewahi kufuzu mara moja tuu, tena naona ni kwa bahati tuu maana ilipoenda ilikuwa ya kwanza kuvungasha virago kwenye raundi ya kwanza. Taingia hapo hadi leo ni kuvurunda tuu maana timu inaenda kushiriki tuu na sio kushindana kwakuwa bado hatujajipanga ipasavyo.

All in all tuende tukafe kiume chema huko yani ni kufa na kupona ila tuhakikishe tunaenda Gabon 2017 kwa kuichapa Nigeria nyumbani kwao tena magoli mengi na Misri wakija hapa tunawachapa, cha msingi wachezaji watulie, wajipange, wacheze vizuri, kocha atathmini michezo ya awali kwanini tulidraw na kufungwa? apange timu vizuri, hapa unaona kweli ushindi wa stars upo mikononi mwao wenyewe, kwanza Nigeria na Misri viwango vyao vimeshuka kwakuwa walishindwa kufuzu mashindano yaliyopita.
 
Ndoto za mchana kuwafunga misri nje ndani. Japo natamani sana iwe hivyo lakini sio rahisi
 
h

hivi kinacheza kiwango au dhamira, acheni kuwatia watu pressure, waembieni hao wanaosimamia mpira wajenge kiwango na sio kuomba dua wakati miguuni mpira haukai, acheni kufikiria mambo hayo ya kuwashinda MISRI na Naigeria kwa kuomba dua.

Acha kupaniki bila sababu, kama wewe kushinda Misri unaona haiwezekani baki na imani hiyo. Nijuavyo mimi Misri inaweza kufungika hapa nyumbani. Kama tunaweza kumfunga Morocco kwa nini iwe jambo lisilowezekana kwa Misri?
 
Ndoto za mchana kuwafunga misri nje ndani. Japo natamani sana iwe hivyo lakini sio rahisi
Mkuu makutu sio nje ndani tena, kumbuka Stars ilienda Misri baada ya timu yetu kutoka kwenye mashindano ya Cosafa ambako tulipigwa game zote kama sikosei, na kule Misri tukachapwa goli 3-0.
Baadae tukatudi Dar kucheza na Nigeria tukatoa sare, kwahiyo Misri tumebaki nae game moja tutakuwa Home, then tutaenda Abuja- Nigeria kumaliza na Super Eagles. Tukishinda game zote mbili zilizobaki tutakuwa tumekusanya point 7 jumla ambazo tayar Misri Anazo mkononi mpaka time hizi, labda ili tufuzu Afcon 2017 huko Gabon lazima tumpige Misri hapa Dar kwa idadi ya goli kama 3 hivi kwa nunge then tukamchape Nigeria huko huko kwao Kwa idali ya kama goli 2-0 hivi ili tuwe na magoli mengi kuliko Misri.
Ila sidhani kama hilo litawezekana, kwa maana hiyo ni kusema kwamba Misri wameshafuzu tayari kwenye kundi hili.
 
Yote yanawezekana,vijana wakaze misuli.
Kocha Mkwasa dhihirisha Dunia kwamba unaweza.
Kocha mwenyewe Mkwasa anadai mshahara wake wa zaidi ya miezi 6,milioni mia mbili.Morali ataitoa wapi?

Makocha wazungu walikuwa wanalipwa bila kulimbikiziwa mishahara yao lakini kwa kuwa huyu ni mzawa,basi imekuwa taabu!

Sisi watanzania tunaweza mashindano ya ulevi na ngono kama Big brother n.k.
 
Sina uhakika kama tutafika popote juu ya hawa watu..
 
h
ahahahahahahah mkwakwan eee?
 
Ujinga mwingine wa watanzania

Uwafunge misri kwa mpira upi ulionano?

Uwafunge Nigeria kwa mpira gani ulionao?

Kwa uwekezaji upi ulionao

Hii Mizuka itawaua watanzania
 
game zitachezwa lini manake nina morali ya ajabu pumbav alafu isipoonyeshwa live tbc kitaeleweka waaaaaah!
 
Mbona TZ tushatoka muda tu...MISRI ameshafuzu tayari hamna wa kumzuia. kikwazo cha misri alikuwa nigeria sasa amefungwa unafikiri nana atamzuia asifuzu..

mpira ni sayansi sio nadharia tu.... nigeria amewekeza kwenye soka na anawachezaji profeshno, hiki ndicho kilichomuhogopesha misri. TFF haijawekeza kwenye soka pesa zote wajitajirisha ubavu wa kumfunga Misri utoke wapi?
 
Labda malinzi akiondoka pale TFF Ndio tunaweza kufanya maajabu hayo, kocha anadai mishahara zaidi ya miezi 8 sasa,
 
Ili tuweze kupenya (kumbuka ni mshindi wa Kwanza tu ndo atasonga kutoka kundi hili), inabidi tuwabamize Misri bao NNE bila majibu and then tukawabamize Nigeria.

Japo huwa tunajifariji kwamba mpira unadunda, kwa case yetu hali ni tete.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…