David Serikali
Member
- Mar 2, 2012
- 57
- 17
Timu ya taifa ya vijana ya Nigeria, Golden Eaglets chini ya miaka 17 imetwaa ubingwa wa kombe la dunia kwa vijana.
Nigeria iliyofunga Mali katika mchezo wa fainali kwa mabao 2-0 huku mshambuliaji wake Victor Osimhen akitia nyavuni goli la kwanza na Funsho Ibrahim Bamgboye akaongeza goli la pili na la ushindi.Kikosi cha cha vijana cha Nigeria kimeweza kutetea ubingwa wake baada ya kutwaa taji hilo la dunia la vijana mwaka 2013 walipoishinda Mexico kwa mabao 3-0.
Mshambuliaji Victor Osimhen ameibuka mfungaji bora kwa kufunga jumla ya magoli 10 katika michuano hiyo.Afrika ilikuwa imekwisha jihakikishia ubingwa wa dunia baada ya kufika fainali kwa mataifa mawili ya Afrika ambayo ni Nigeria na Mali kufika fainali.
Chanzo: BBC