Nightmare ni nini?

Nightmare ni nini?

Andazi

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2022
Posts
1,113
Reaction score
2,234
Nimekuwa nikisikia sana huu msamiati, kwangu ninachoelewa ni kuwa ni ndoto za kutisha.

Kuna maana nyingine nje ya hapo au ni tofauti na ndoto au ni dubwana linalosababisha kitu kwenye ulimwengu wa ndoto?

Kwa taadhima tuwakalibishe wazee wa kilinge tupate jambo, msitegeane, na yeyote mwenye elimu ambaye sikumtaja hapa;

Rakims
Herbalist Dr MziziMkavu
Mshana Jr

NB: Mahubiri ninayajua, so hapa nisingependa kuyasikia.
 
Hilo ni neno la kingereza mixer na kijaluo
Night = usiku
Mare = wake/yake/chake
Kwahiyo likiunganishwa neno zima ni nightmare kwa tafasiri ya kiswahili ni usikuwake.
Sasa hapo mkuu, kwanini usipate mapicha picha mixer unapoleta uzi mida wa wanga...🤔
 
Ni ndoto ambayo inakuwa unahisi kukabwa au km unashikiliwa na kitu mwilini mzima kama ume paralyse unashidwa kuongea ni ndoto ambayo mtu akiota lazima ashtuke kiufupi
 
Ni jinamizi ama majinamizi. Jinamizi ni kiumberoho kinachojengewa sura ya kutisha na kukutokea ukiwa umelala. Lakini kiuhalisia hakuna kiumbe kama hicho bali ni mambo ambalo huumbwa na mhusika kwa muktadha binafsi kutokana na hofu mbalimbali zinazomkabili katika harakati za maisha.

Ama kulala vibaya na kuzuia hewa kupita vizuri kooni, kulala chali na kulifanya jicho la tatu kuona vitu mbalimbali vya kutisha ama kushiba sana. Vilevile kuna majinamizi kutokana na mambo ya kishirikina.
 
Sasa hapo mkuu, kwanini usipate mapicha picha mixer unapoleta uzi mida wa wanga...[emoji848]
Ndoto ni njia ya ubongo wetu ya kupanga matukio ya siku, kumbukumbu, na picha kuwa hadithi za wazi, za mfano, na zisizo na maana.” jinamizi(nightmares) ni "ndoto ambazo mara nyingi huunganishwa na wasiwasi ambao haujatatuliwa na kiwewe ambacho ubongo wetu haujashughulikia kikamilifu."
 
Hilo ni neno la kingereza mixer na kijaluo
Night = usiku
Mare = wake/yake/chake
Kwahiyo likiunganishwa neno zima ni nightmare kwa tafasiri ya kiswahili ni usikuwake.
Sasa hapo mkuu, kwanini usipate mapicha picha mixer unapoleta uzi mida wa wanga...🤔
Aaaaaa sawaa
Ni ndoto ambayo inakuwa unahisi kukabwa au km unashikiliwa na kitu mwilini mzima kama ume paralyse unashidwa kuongea ni ndoto ambayo mtu akiota lazima ashtuke kiufupi
Oooohoooo
 
Ni jinamizi ama majinamizi. Jinamizi ni kiumberoho kinachojengewa sura ya kutisha na kukutokea ukiwa umelala. Lakini kiuhalisia hakuna kiumbe kama hicho bali ni mambo ambalo huumbwa na mhusika kwa muktadha binafsi kutokana na hofu mbalimbali zinazomkabili katika harakati za maisha.

Ama kulala vibaya na kuzuia hewa kupita vizuri kooni, kulala chali na kulifanya jicho la tatu kuona vitu mbalimbali vya kutisha ama kushiba sana. Vilevile kuna majinamizi kutokana na mambo ya kishirikina.
Ndio maana ninaogopa kulala chalii
Ndoto ni njia ya ubongo wetu ya kupanga matukio ya siku, kumbukumbu, na picha kuwa hadithi za wazi, za mfano, na zisizo na maana.” jinamizi(nightmares) ni "ndoto ambazo mara nyingi huunganishwa na wasiwasi ambao haujatatuliwa na kiwewe ambacho ubongo wetu haujashughulikia kikamilifu."
Aaaa ahsante kwa elimu
 
Nightmares ni ubwabwa boko boko uliopikwa kwa mafuta ya transformer
 
Back
Top Bottom