holoholo
JF-Expert Member
- May 10, 2023
- 1,859
- 2,986
Wakuu,
Kuna binti kijiji jirani toka nilipo mimi,nilimpenda sana nae akanipenda sana,
Ilifikia hatua nikamnunulia simu, tukawa tunawasiliana, mapenzi yakakolea wakuu,binti kila anaekuja kuchumbia anamkataa,mpaka wazazi wake wakakaa nae kitako, wakamuuliza kama unakataa kuolewa je unataka uolewe na nani?
Akajibu nataka kuolewa na holoholo ikabidi nitafutwe na wazazi wa binti, ishu nikaikubali,wakaniambia nikajitambulishe, nikagoma
Katika matumizi ya simu binti alikuwa anatumia kwa siri sana,ila badae akaja akagundulika kuwa anatumia simu,akabanwa akasema kuwa nimempa mimi, akanyang'anywa, nikapigiwa simu niifuate nikagoma
Binti akaondoshwa pale nyumbani akapelekwa wilaya tofauti na ninayoishi mimi ila akawa ananipigia simu kwa siri, baadae akapatikana mchumba,binti akakataa katakata kuolewa lakini akalazimishwa kuolewa, binti akaolewa
Nipo katika dilema je niifuate simu yangu kwa wazazi wa binti au niipotezee.
Ushauri wenu wakuu
NB: stori hizi ninazoleta jukwaani si za kutunga.