Mr George Francis
JF-Expert Member
- Jun 27, 2022
- 278
- 512
Neno linasema, "NIITE NAMI NITAKUITIKIA, NAMI NITAKUONYESHA MAMBO MAKUBWA, MAGUMU USIYOYAJUA."
Neno la Mungu katika kitabu cha YEREMIA linatuonesha kwamba nabii Yeremia alikuwa mfungwa wakati huo.
Alikuwa amefungwa ndani ya uwanda wa walinzi, uliokuwa katika nyumba ya mfalme wa Yuda na wakati huo jeshi la mfalme wa Babeli liliuzunguka mji wa Yerusalemu.
Mji huo wa Yerusalem ulikuwa karibu kuanguka, na watu walikuwa wameasi Mungu kwa miaka mingi.
Hali ilikuwa ya huzuni, hofu na kutokuwa na tumaini juu ya maisha yao.
Katika hali hiyo ngumu, Mungu anamwambia Yeremia na kupitia yeye, anatuambia sisi leo kwamba
"Niite nami Nitakuitikia, nami nitakuonyesha mambo makubwa, magumu usiyoyajua."
Hapa kuna maneno matatu muhimu ambayo tunapaswa kuyatafakari kwa kina sana.
1. "NIITE" - Hii ni amri + mwaliko. Mungu anasema: “Niambie nije kwako ili uongee nami, uzungumze yaliyo moyoni mwako."
Ni sawa na leo atokee tajiri kama Mohamed Dewji akwambie George, au Maria niite nije ulipo ili uniombe msaada.
Neno "Niite” maana yake usikae kimya, usikate tamaa, usijaribu kutatua mambo peke yako. Niambie nije ili unishirikishe shida zako.
Mungu anaju shida zako lakini anataka tumuite ili aje tumwambie shida zetu moja kwa moja kupitia maombi, dua na sala.
Sio lazima uwe na maneno mazuri au maombi marefu ila yeye anataka uhusiano wa karibu kati yetu na yeye kama mtoto na baba yake.
2. "NAMI NITAKUITIKIA.” - Mungu hawezi kusema umuite alafu akakupuuza.
Yeye ukishamuita anakusikia na anakuitikia au anakupa majibu.
Jibu lake linaweza kuwa “Ndiyo”, “Subiri”, au “Nimekupa kitu bora zaidi ya hiko unachokiomba wewe.”
Lakini Mungu hakosi kuwa na jibu.
Kumbuka: Mungu hajibu kila wakati kama tunavyotaka, bali kama anavyojua kuwa ni bora zaidi kwetu.
Mungu awahi wala achelewi lakini anajibu kwa wakati sahihi ule autakao.
3. "NAMI NITAKUONYESHA MAMBO MAKUBWA, MAGUMU USIYOYAJUA ” - Hii ndiyo sehemu yenye nguvu sana ambayo tunapaswa kuielewa kwa umakini mkubwa.
Mungu anasema atatuonyesha
● Mambo makubwa. (Haya ni yale yaliyo juu ya uwezo wako wa kawaida.
● Mambo magumu. (Haya ni mambo ambayo akili yako peke yake haiwezi kuyafikia au kuyaelewa.)
● Mambo tusiyoyajua. (Haya yaweza kuwa ni siri, mipango, suluhisho, au baraka ambazo bado hazijaingia akilini mwako.)
Hii inamaanisha kwamba wakati unapomwita Mungu kwa bidii, Yeye hufungua macho yako na moyo wako kuona na kuelewa mambo ambayo hujawahi kuyafikiria.
FUNZO KUU TUNALOPATA NI KWAMBA:
Maombi si jambo la mazoea bali ni mazungumzo halisi na Mungu aliye hai. Mungu anataka tuwe karibu na yeye kupitia maombi na sala.
Hata katika shida kubwa, Mungu yuko tayari kujibu. Yeremia alikuwa gerezani, lakini Mungu alimpa tumaini la mustakabali mzuri wa taifa lake licha ya magumu waliyopitia.
Vivyo hivyo, hata kama uko “gerezani” kama Yeremia yaani gereza la shida mbalimbali (ugonjwa, fedha, mahusiano, hofu, kutopata kazi, ndoa, maamuzi makubwa n.k.), Mungu anasema "NIITE NAMI NITAKUITIKIA."
Mungu ana mambo makubwa ambayo anataka kukufunulia. Usikae na mawazo madogo tu. Omba kwa imani, na Yeye atakupa ufahamu, hekima, au maono mapya ambayo hayatokani na wewe mwenyewe kwa akili zako.
Ebu fikiria leo tajiri mkubwa au Kiongozi mkubwa katika nchi akwambie niite nami nitakuitikia je ni nani kati yetu atakataa fursa hii?
Sasa kwanini Mungu anakwambia niite nawe unashindwa kufanya hivyo? Tena kwa vijisababu ambavyo havina hata mashiko.
Nakuhusia wewe na kuihusia nafsi yangu kuanzia leo hii tutenge muda wa kusali na kuomba kila siku, asubuhi, jioni au hata katikati ya usiku mzito ukipata nafasi ya kushtuka usingizini usikimbilie TikTok au Facebook.
Shika kitabu chako kitakatifu (biblia au msaafu) soma neno la Mungu kisha omba kwa imani yako chochote unachotaka naye Mungu atakuitikia na kujibu maombi yako.
Tumsifu Yesu Kristu, .....
Assalamu alaikum .....