Vodacom sijui kimewapata nini huu mtandao nilikua naupenda sana zamani ila siku hizi naona wamekua km ule mtandao ulikua unajifia wenyewe ukajipachika kwa Tigo wanaitwa nini sijui Zantel, sasa hivi mitandao giant's ni mitatu tu Airtel, Tigo/Yas na Halotel ila Vodacom anashika mkia, Vodacom sijui nini kimewapata yaan Vodacom inashika vizuri maeneo ya mjini mjini tu ukiingia machakani maporini huko kwakheri umeisha.. funiko ni Halotel na Yas na Airtel kwa mbaali ingawa Airtel nao wanazingua inakata network haisomi, nakumbuka kuna eneo nilifika nikiwa natokea Mwanza hakuna mtandao kabisa eneo hilo ni miti tupu porini kabisa chaka vibaya sana gari ikawa imekula pancha nikaanza kuusaka mtandao weka simu juu juu Halotel ikasoma nikapiga simu nikaongea
Ps: Haya ni maoni yangu binafsi sio maoni ya watumiaji wote wa mtandao..