Mwaka huu by mwezi wa 9/10 natarajia nikaanza uuzaji wa MBEGU ZA VITUNGUU original red Bombay kile chenye uzambarau wanapenda wakenya na kina bei sokoni kwa bei nzuri naahidi nitakuwa mwaminifu maana watu wanafanyiwa ujinga kwenye mbegu kumiksiwa makapi n.k mwisho wa siku mavuno hafifu na vitunguu kuchanua mabomba.
yeyote anayetaka au anayelima kitunguu awe makini sana kwenye mbengu maana haitakiwi upate segere kizembe.
Zifuatazo ni mbinu za kutambua mbegu fake na iliyochakachuliwa.
*chota na mkono toka nje lakini angalia mbegu isipokuwa nyeusi tiii na ukiona mbegu zenye kufifia uweusi umepigwa.
*Kuna mbegu makapi Zinaoshwa huwa nizakutupwa Ila wahuni wanachanganya hizi kuzitambua kwa mtabe akinusa tu anajua ila kwa MTU wa kawaida chukua kiganjani kidogo isugua like kupekecha makapi utaona inasagika mbegu nzur ni ngumu.
*Chukua mzani pima kilo za mbegu debe itoe kg11 paka 12 ikiwa chini ya hapo kuna walakini ila watz huwawezi kuna namna wanamix na tumawe flani mfanano wa mbegu copy right hahahhaha hapa lazima ukae nitaelezea baadae kuruka viunzi hivi.
*Unaweza kupepeta mbegu kwenye upepo wa wastani kwakumwaga taratibu mbegu itakayotua miguuni kwako it means ni nzito na ilienda distance kidogo ni nyepes hivyo inaenda kwa grade kutoka ya centre ndo the best unavyomove mbele ndo ubora unapungua paka zilizopeperushwa mbali hayo makapi.Makapi ndo hutoa vitunguu dhaifu vidogo visivyoeleweka na kama ukipanda mbegu inayotua centre ile nzito grade one only utavuna paka utachanganyikiwa ila kuipata paka uisort mwenyew japo hii package naifikiria nikianza biashara panapo majaaliwa