Mi nakunywa maji ya uvuguuvugu lita moja asubuhi kabla sijala wala kuswaki na usiku lita moja kabla ya kulala,mara nyengine nachanganya na limao na kijiko kimoja cha asali mbichi.
Faida za maji nilizoziona kwangu ni
1.Kuchangamsha mwili hususan asubuhi,nikinywa huwa inaondoa kabisa ule uchovu wa asubuhi pamoja na usingizi
2.Ina lainisha choo
3.Inasaidia kusafisha tumbo
4.Kupunguza mafuta mwilini
5.Inasaidia mmengenyo wa chakula.
6.Kutibu mafua na kifua,kuumwa kichwa etc
Kwa kifupi maji ni dawa kubwa kuliko dawa nyengine zote.jitahidi kunywa walau lita mbili au zaidi kwa siku.Pendelea kunywa maji ya uvuguuvugu,maji ya baridi sio mazuri kiafya.