Nikashangaa kama waliomuua mtumishi TRA watajulikana kabla ya wauaji wa Mzee Kibao

Nikashangaa kama waliomuua mtumishi TRA watajulikana kabla ya wauaji wa Mzee Kibao

ngara23

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2019
Posts
9,091
Reaction score
21,087
Kwanza nalaani haya mauaji yote
Mauaji yote chanzo ni hapo Tegeta
Wananchi kuchukua sheria mikononi na kuuwa sio jambo zuri, wote tunalilaani

Mzee Kibao alikufa Toka mwezi September hadi Leo hatujaona hao watekaji na wauaji wa Mzee Kibao kukamatwa na japo waliacha kila alama.

Mzee Kibao alitekwa mchana kabisa watu wanaona, kwenye bus Tashrif alikuwepo askari na majina yake yalitajwa, hao watekaji walikuwa na bunduki na pingu.

Kama hawa hawajajulikana ina maana hatuko salama kama Taifa

Sasa huyu mtumishi wa TRA aliuawa na watu waliomtilia shaka kuwa ni Moja ya watekaji, ambapo watekaji nao wanakuja na tabia hizo sio police na hawana vibali vyovyote na hili liliwapa wananchi hasira na kuchukua sheria mikononi

Nitashangaa kama hatua zitachuliwa dhidi ya hawa wauaji wa mtumishi TRA kabla ya wale wa Mzee kibao

Hapa ndo tutapima utashi wa serikali na kuona raia wote ni sawa, na tutaona haki

Pia soma
 
Back
Top Bottom