Iwashe kwanza na baada ya kuunguruma kwa muda mfupi ifunge mafuta , lakini uiache ikiunguruma mpaka mafuta yaishe kwenye kabureta na itazima , unafanya hivyo kwa sababu mafuta yakiwapo kwenye kabureta yatasababisha jet za mafuta kuziba. Baada ya hapo fungua terminal ya -ve ya battery ya pikipiki yako. Ukirudi unga hiyo terminal fungulia mafuta washa pikipiki . Hii ni kwa uzoefu wangu wa kutumia pikipiki muda mrefu.