Wakuu,
Mimi hua nikiangalia bunge letu naona wachekeshaji tu na watu wenye vioja na mzaha mwingi yaani ile dhana ya wawakilishi inafia hapo.
Hua najiuliza hawa jamaa wanaenda mule ndani na mawazo yao au mawazo ya wananchi?
Haiwezekani tozo ipitie kwao wapitishe sheria baadae wananchi wanaikataa inarudi kwao halafu na wanaipitisha tena kuikataa halafu baadae wanapiga makofi, hii ni kupoteza muda wa wananchi waliowatuma kule kwani ina maana hawakuona mwanzo kama hazifai?
Kazi yake kule ni kuwasilisha mawazo ya wananchi lakini pia kuisimamia serikali lakini wao hugeuka wasifiaji na watetezi wa serikali hiyohiyo muda wote. Nadhani matokeo ya kua na wabunge wa chama kimoja ndio matokeo yake hayo wanakosa msuguano wa hoja na kufanya wanavojisikia.
Wananchi sasa waamke wasipeleke bora mwakilishi wapeleke mwakilishi mwenye viwango vya juu kuwawakilisha bila kujali chama anachotoka kikubwa awe na uwezo tu.