Nikiendesha Gari inakula mafuta hatari

Wakuu nisaidieni kuelewa kitu nikiendesha gari inakula mafuta sana tofauti na mtu mwingine akiendesha gari hiyo hiyo, Nashidwaa kuelewa ni nakanyaga vibaya pedel ya mafuta au kuna kitu nakosea, msaada wenu wakuu.
Cheza na Engine Rotation isizidi 3,000, jitahidi uiche gari iongeze mwendo yenyewe.....ndio mtazamo wangu huo
 
Very professional reply!! Uko Speed 60 huku RPM Iko 3000 lazima itakutesa
 
Cheza na Engine Rotation isizidi 3,000, jitahidi uiche gari iongeze mwendo yenyewe.....ndio mtazamo wangu huo
Kwa dar 2000 rpm zinatosha kabisa, labda kama unapanda kilima ndo unaweza sogea mpaka 3000. Sema huyu usikute ana subaru impreza zile hatchback. Accelerator nyepesiiiiii na ukiweka economy mode inakuwa very slow causing one to press harder on the accelerator pedal.
 
Yaani huo mlima labda awe na bonge la mzigo ndio aifikishe huko 3,000! Ni driving behavior tu ndio inayomtesa! Gari Haina shida
 
Nimewaelewa wakuu hebu nisaidieni nimesikia position ya kiti cha dereva pia inachangia mimi huwa napenda kurudisha kiti nyuma kabisa nakanyaga mafuta mguu ukiwa umenyooka kabisa hii inaweza kuchangia ulaji mbovu wa mafuta?
 
Wakuu nisaidieni kuelewa kitu nikiendesha gari inakula mafuta sana tofauti na mtu mwingine akiendesha gari hiyo hiyo, Nashidwaa kuelewa ni nakanyaga vibaya pedel ya mafuta au kuna kitu nakosea, msaada wenu wakuu.
Unatakiwa uwe soft foot dont be too hard on gas!

Sikilizia mapigo ya engine..kanyaga softly gari itabadili gears haraka haraka na itakamata kasi bila shida.

Maintain RPM below 2000 Revolutions Per Minute. Hakikisha unapokanyaga mshale hauvuki namba 2 gari ibadili gear smoothly.

Ukigandamiza mguu gari ikavuka zaidi ya 2 RPM inashikilia gear moja mda mrefu inahisi iko mlimani au unataka overtake,,,kumbe iko tambarare tu hili kosa wengi hufanya baada ya kupanda tuta na kushuka.

Ukiweza maintain below 2 utanipa majibu namna gari inavyokula vizuri
 
Pia jaribu kuangalia na mfunobwa umeme yaani plugs na kabureta, otoneta nk, mfumo wa upumuaji wa gari yaani air cleaner nadhani utapata jibu
 
Asante sana mkuu nimeijaribu hii idea leo
imefanya kazi nashukuru kwa ushauri
 
Khaaa🤣🤣🤣aisee hii nchi ngumu sana? Sasa atumie nini kuaccelerate? Handbrake au?
Mita cha he mbele unakata kona kuingia nyumbani, mguu bado upo kwenye mafuta, unafika kwenye kona ndio unapiga break......hapo vipi?
 
Asante sana mkuu nimeijaribu hii idea leo
imefanya kazi nashukuru kwa ushauri
Sasa wewe hata kushuka mlima kitonga unashuka huku mguu umekanyaga mafuta unategemea nini?

Mimi kwa siku naweza kupunguza mpaka kilometer kadhaa gari nikishachochea unatowa mguu kwenye mafuta inakwenda yenyewe.

Ukiwa na tabia hiyo unajikita kwa siku umesave kilometer kadhaa na ukikanyaga sio mpaka kibati, ni soft touch kama vile kuna miba unaogopa isikuchome.
 
 
Mita cha he mbele unakata kona kuingia nyumbani, mguu bado upo kwenye mafuta, unafika kwenye kona ndio unapiga break......hapo vipi?
Hapo fresh. Si ushafika. Shida ingekuwa unahitaji kuaccelerate tena.
 

Thread ilitakiwa iishie hapa...

Labda tu kitu kingine cha kumuongezea, ni aina ya barabara anazopita (options za barabara anazochagua kupita)...

Huenda anapita sana chocho hivyo huongeza kilometer na gari muda mwingi kuwa kwenye gia ndogo...huenda pia huchagua njia zenye vilima sana...au pia mida anayoendesha yeye huwa ni zile busy hour...
 
Pole sana, ngoja waje kukupa muongozo...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…