"Nikifanya kazi moyo unaendaaa mbioo nikiinamaa sanaa nikisimama sana piaa nikitembeaa sana au nikipataa mshtukoo tu basi unaanza kwenda mbio pia nikiwa na mawazo."
Ushauri wa kitaalam unahitajika kwa haraka.
Pole kwa kuumwa.
Kwa jinsi unavyoeleza kuna mambo matano naweza kutaja kuwa yanahitaji kutazamwa vyema:
1: Kiasi cha damu
Upungufu wa kiasi cha damu huweza kupunguza uwezo wa mwili kulicha viungo vyake chakula na oksijeni, hivyo katika jitihada za mwili kujisahihisha hivyo kuleta dalili tajwa.
2: Moyo
Kuna matatizo mengi ya miyo yanaweza kuleta dalili husika mfano: tatizo la moyo kutanuka, tatizo la valvu na tatizo la kianzisha mapigo ya miyo nk. Hii husababisha moyo kutokuweza kusukuma damu ya kutosha kwenda kwenye mwili.
3: Mapafu
Kuna matatizo yanayoweza kuhusisha mishipa ya damu ya mapafu na maumbile yake kwa ujumla. Hii hufanya mzunguko wa damu toka kwenye moyo kwenda kwenye mapafu na kutoka kwenye mapafu kurudi kwenye moyo kutokuwa sawa na wa kuridhisha mahitaji ya mwili.
4: Saikolojia (Stress vs Anxiety)
Hii huweza kusababisha homoni/vichocheo kuwa juu, hasa vinavyohusika na kupeleka moyo mbio.
Pia hili huweza kufanya usile vyema na kupumzika vyema yote hayo kukufanya usiwe mwenye nguvu. Hii huchochea mzunguki wa stress-anxiety-poor rest-poor eating habit-poor performance -anxiety.
5: Presha yako
Unaweza kuwa ni mtu mwenye presha ya chini/kushuka. Hivyo, unapokuwa na njaa, uchovu au moyo kwenda mbio kwa sababu moja au nyingine hapo juu basi, hilo husababisha mwili kutokupata chakula na oksijeni kutosha.
NB: Ili kupata jibu sahihi na tiba sahihi ni vyema kufika hospitali na ujieleze vyema yale yote ambayo hayako sawa kwenye mwili wako.
Mtoa huduma ya afya atategemea zaidi maelezo yako na atakuangalia pia kuomba vipimo iki kuthibitisha au kukanusha baadhi ya mawazo atakayokuwa nayo. Na baada ya hapo mtakubaliana juu ya hatua ya tiba.