Mwenzenu najijutia, Nawahi kukufuru Mungu kwa nini nilizaliwa.
Lakini sawa. Mola ndivyo alivyotupangia. Jambo akipanga Mola vigumu kulipangua.
Kinachoniuma roho nikimtizama mwanangu Pili anavyonitegemea
Huwa najiuliza sana kitu gani nitamgaia.
Au nitakapofariki mwanangu urithi gani nitamuachia. Najua atapata tabu sana hapa katika Dunia. Nawaza liwalo na liwe. Hayo yameshatokea hakuna la kufanya kuweza kuniokoa.