Nikikuchangia Laki Bwana Harusi Ukumbini nitegemee kupata nini?

Kaunara

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2013
Posts
249
Reaction score
452
Habari wadau?

Kuna jambo linanikwaza sana. Unakuta mtu ana harusi. Anaomba mchango kama deni vile! Unamchangia mtu laki ukiingia ukumbini mtu unapewa kifungashio cha juice na soda hata elfu kumi haifiki.

Inakuwa tena kama tunampa mtaji bwana harusi. Jipange bwana harusi ndo uombe hela.
 
Hii tabia ya kuchangishana harusi sijui watu weusi tutaicha lini.

Sijawahi sikia muarabu/muhindi/mzungu akichangisha sababu ya harusi. Na wengi wao hushangaa pale mtu mweusi anapotoa kadi ya kuomba mchango wa harusi.

Ifikie wakati tufanye kilicho ndani ya uwezo wetu. Sio lazima wote tuwe na harusi za kifahari ikiwa ni makapuku.

Raha moja ya waislam, ni kuwa na harusi simple sana. Ukiamua ni kuita watu wachache, maandazi na chai ndoa inafungwa na maisha yanaendelea.
 
Mimi nilishaapa sitochangia mtu mchango wa sherehe ya aina yoyote ile,
Umeamua kuoa pambana na taabu zako,kwani aliesema ukioa lazima sherehe kubwa nani,kuna jamaa alioa na baada ya sherehe alibaki na deni la milioni 12,ingali maisha yake ni duni
Siku hizi mpaka ubarikio mtu anakuomba mchango,mimi nawaonaga wapumbavu tu, unakusudia kufanya sherehe jipange wewe binafsi
Yanakera sana haya mambo
 
Wanachangisha vizuri tu. Jua class ipo sehemu zote kuna mwarabu,muhindi,mzungu maskini pia
Hii tabia ya kuchangishana harusi sijui watu weusi tutaicha lini.

Sijawahi sikia muarabu/muhindi/mzungu akichangisha sababu ya harusi. Na wengi wao hushangaa pale mtu mweusi anapotoa kadi ya kuomba mchango wa harusi.

Ifikie wakati tufanye kilicho ndani ya uwezo wetu. Sio lazima wote tuwe na harusi za kifahari ikiwa ni makapuku.

Raha moja ya waislam, ni kuwa na harusi simple sana. Ukiamua ni kuita watu wachache, maandazi na chai ndoa inafungwa na maisha yanaendelea.
 
Hii tabia ya kuchangishana harusi sijui watu weusi tutaicha lini.

Sijawahi sikia muarabu/muhindi/mzungu akichangisha sababu ya harusi. Na wengi wao hushangaa pale mtu mweusi anapotoa kadi ya kuomba mchango wa harusi.

Ifikie wakati tufanye kilicho ndani ya uwezo wetu. Sio lazima wote tuwe na harusi za kifahari ikiwa ni makapuku.

Raha moja ya waislam, ni kuwa na harusi simple sana. Ukiamua ni kuita watu wachache, maandazi na chai ndoa inafungwa na maisha yanaendelea.
Wazungu wanachanga kistarabu huwa wanafanya party munaailkwa party unaachia envolope yako na jina lako ambayo ndani muna pesa so wanayo michango yao.
 
''Usiache mbachao kwa msala upitao '' kama unayo toa kumpa pushi mtu afurahi ndio maisha hayo , pesa kama ipo toa ...Mimi binafsi siwezi kuandaa sherehe zile heka heka hata graduation sijawahi kifanya tangu nizaliwe.
 
Hii tabia ya kuchangishana harusi sijui watu weusi tutaicha lini.

Sijawahi sikia muarabu/muhindi/mzungu akichangisha sababu ya harusi. Na wengi wao hushangaa pale mtu mweusi anapotoa kadi ya kuomba mchango wa harusi.

Ifikie wakati tufanye kilicho ndani ya uwezo wetu. Sio lazima wote tuwe na harusi za kifahari ikiwa ni makapuku.

Raha moja ya waislam, ni kuwa na harusi simple sana. Ukiamua ni kuita watu wachache, maandazi na chai ndoa inafungwa na maisha yanaendelea.
Kama kipato cha hapa na pale utakula maandazi tu. Usiukaze msuli wakati upaja mdogo.

Ulifuatilia harusi ya binti wa Hussein Mwinyi? Uliona maandazi?
 
Habari wadau?

Kuna jambo linanikwaza sana. Unakuta mtu ana harusi. Anaomba mchango kama deni vile! Unamchangia mtu laki ukiingia ukumbini mtu unapewa kifungashio cha juice na soda hata elfu kumi haifiki.

Inakuwa tena kama tunampa mtaji bwana harusi. Jipange bwana harusi ndo uombe hela.
Namba ya Bibi harusi
 
Hawa
Hii tabia ya kuchangishana harusi sijui watu weusi tutaicha lini.

Sijawahi sikia muarabu/muhindi/mzungu akichangisha sababu ya harusi. Na wengi wao hushangaa pale mtu mweusi anapotoa kadi ya kuomba mchango wa harusi.

Ifikie wakati tufanye kilicho ndani ya uwezo wetu. Sio lazima wote tuwe na harusi za kifahari ikiwa ni makapuku.

Raha moja ya waislam, ni kuwa na harusi simple sana. Ukiamua ni kuita watu wachache, maandazi na chai ndoa inafungwa na maisha yanaendelea.
Hao ni waislam makapuku angalia harusi ya Binti wa mwinyi kama utaona maandazi na chai
 
Habari wadau?

Kuna jambo linanikwaza sana. Unakuta mtu ana harusi. Anaomba mchango kama deni vile! Unamchangia mtu laki ukiingia ukumbini mtu unapewa kifungashio cha juice na soda hata elfu kumi haifiki.

Inakuwa tena kama tunampa mtaji bwana harusi. Jipange bwana harusi ndo uombe hela.
ukinichangia laki mm kamq bwana harusi ntakupa mama mkwe wangu uondoke naye😅🤣😂
 
Back
Top Bottom