Nikikumbuka hii kauli huwa naumia sana

Nikikumbuka hii kauli huwa naumia sana

Kipangaspecial

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
20,778
Reaction score
28,722
Nikikumbuka hii kauli mwili wangu wote unakufa ganzi kwa dakika

Ukiweka Laki Tatu, Baada Ya Week Unaleta Wenzako Wawili Na Wenyewe Wataleta Wawili, Then Baada Ya Mwezi Utaanza Kuingiza Milioni Tatu Kila Week Pia Utaweza Kwenda Spain Kwenye Semina Zetu - GLOBAL ALLIANCE

Laki 3 zangu zikawa zimeenda bureee, mshamba mimi nikawa nimeibiwa

Sijajua wenzangu mliowahi kukutana na kauli kama hii mliichukuliaje.
 
Pole sana mkuu kila mtu alishapigwa kwa wakati wake.

Mimi nakumbuka nilipigwa na Tapeli anajiita mganga kutoka Tanga anatibu UKIMWI kwa kutumia majini. Nilikuwa na rafiki yangu wa kike aliyeathirika na kwa kuwa alikuwa rafiki wa kufa na kupona nilijitahidi sana kutafuta tiba kwa namna yoyote

Nilikutana na Huyu anaitwa Yunus Manzi tapeli mkubwa akala laki mbili zangu enzomi hizo.

Nilikuwa mpumbavu kumbe ukimwi hauponi.
 
Sijawai kukamatika kwenye hili, nakumbuka mwaka 2016 marafiki zangu watatu wakisukuma walishawishika wakaingia na wenza wao wakawakusanya na baadhi ya ndugu zao wakiamini kwamba wanauaga umaskini jumla.

Mmoja wao alishawai kunishawishi sana akaniambia bwana fulani mimi after two weeks nanunua gari nawewe kama rafiki yangu ningependa ufanikiwe kama mimi naomba tuwe pamoja jiunge, nilikataa na hadi sasa yule Bwana kawa kama tapeli gari ad leo hajafanikiwa na maisha yanazidi kuwa magumu kwake ila kuna kitu kinanishangaza mbona wengi wao hawaachi?
 
Back
Top Bottom