Nikimeza kitu chochote naumwa kooni

KMMS

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2017
Posts
304
Reaction score
586
Wanajamvi Mungu ni Mkuu bado twapumua;

Kama nilivyotangulia kudokeza hapo juu,nikwamba nimekuwa nikipata shida sana (maumivu) nikimeza kitu chochote
.
Eneo la kidaka tonge! Ni kwa siku mbili mfululizo,Yani maumivu haya yananinyima raha sana,mbaya zaidi nipo eneo ambalo kupata huduma ya kitabibu ni shida maana ni kijijini sana.

Tafadhali kupitia jukwaa hili la JF Doctor naomba kupata msaada wa kitabibu.

Natanguliza Shukrani....!
 
Mkuu pole sana hyo yawezekana ikawa tonsils jaribu kusukutua na maji ya uvuguvugu yaliochanganywa na chumvi. Maumivu yakizidi pata ushauri wa daktari.
 
Jaribu kutumia antibiotics, anza na Clavulin siku tano kwanza zisipotibu rudi hapa hapa
 
Shukran Wakuu,Nafanyia kazi ushauri wenu.
 
Mimi nimeshawah kuumwa hivyo nikaenda hospitali nikapewa magnesium nikatumia nikapona
 
Una maumivu au uvimbe chini ya masikio kuzunguka shingo? Infection ndiyo sababu kubwa ya maumivu wakati wa kumeza kitu.
 
Una maumivu au uvimbe chini ya masikio kuzunguka shingo? Infection ndiyo sababu kubwa ya maumivu wakati wa kumeza kitu.
Nashukuru nilipata ushauri humu,Nilitumia njia ya asili kwa kusukutua,Now naendelea vyema!

Shukrani nyote kwa Ushauri.
 
Mi pia nilikua nayo juzi sasa jana naamka imepoa ila nashangaa shingoni kuna swollen lymph nodes .....sasa najiuliza sababu ni hyo hyo au......na itaisha lini hii nodes...

Note. Hii vidonda kooni ilikuja baada tu ya kupata kiungulia kikali sana
 
Daaaah ni ninayo hyo Sky Eclat ilianza kiungulia kikali, baada ya kuisha nikapata hiyo sore throught kumeza kitu ilikuwa tabu.sa hv imeisha kumetokea uvimbe shingoni kwa juu chini ya sikio....

Yote hayo ndani ya week moja tu
Una maumivu au uvimbe chini ya masikio kuzunguka shingo? Infection ndiyo sababu kubwa ya maumivu wakati wa kumeza kitu.
 
Daaaah ni ninayo hyo Sky Eclat ilianza kiungulia kikali, baada ya kuisha nikapata hiyo sore throught kumeza kitu ilikuwa tabu.sa hv imeisha kumetokea uvimbe shingoni kwa juu chini ya sikio....

Yote hayo ndani ya week moja tu
Mkuu nenda hospitali usiichukulie poa, uvimbe unaweza kuwa ni tezi za immune system chini ya masikio zina respond.

Cancer ya oesophagus ni hatari, wahi hospitali.
 
Mkuu nenda hospitali usiichukulie poa, uvimbe unaweza kuwa ni tezi za immune system chini ya masikio zina respond.

Cancer ya oesophagus ni hatari, wahi hospitali.
Duuuuhh mpka nimsisimka aisee...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…